Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA YACHOMOA MBELE YA MTIBWA


Mshambuliaji wa Yanga,Hamisi Kiiza akipiga shuti mbele ya beki wa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Taifa,Jiji Dar es Salaam,katika Mechi iliyoishia kwa Yanga 1-1 Mtibwa Sugar

Beki wa Mtibwa akijitahidi kula sahani moja na Kiiza aliyekuwa mwiba mkali kwa beki ya Mtibwa ambao mara kwa mara alikuwa akibisha hodi langoni mwao.

Jerry Tegete akijaribu kufunga lakini kipa wa Mtibwa Sugar Hussein Sharrid'Casillas' akizuia mchomo huo


Mfungaji wa bao la Mtibwa Sugar,Shaaban Kisiga'Malone' akimiliki mpira mbele ya viungo wa Yanga,Athumani Iddi'chuji' na Mbuyu Twite(kulia)

Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakipongezana baada ya Kisiga kuipatia timu baoHamisi Kiiza(wa pili kutoka kushoto) na Said Bahanuzi ambao walianzia bechi kabla ya kuingia na kufanikiwa kuisawazishia Yanga 

Golikipa wa Mtibwa akiondoa mpira wa hatari langoni mwake

Golikipa wa Mtibwa Sugar akiondoa mpira miguuni mwa Tegete aliyekuwa anaelekea kufunga goli.


Didier Kavumbagu akiwa amefanikiwa kumtoka kipa lakini akapiga nje ya Lango katika mshangao wa wengi

Kavumbagu akimlamba kipa wa Mtibwa Sugar chenga

Tegete liwekwa chini ya Ulinzi mkali leo

Tegete akiwa hana la kufanya baada ya kushindwa kutumbukiza mpira wavuni huku golikipa nae akiwa ameukodolea macho.
Haruna Niyonzima akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Mtibwa

Casillas akizuia shuti la Msuva


Msuva akimtoka Issa Rashid 'Baba Ubaya' ambae alikuwa na kazi nzito leo mbele ya wachezaji wa Yanga 'Wazee wa Uturuki'

Wachezaji wakiwa hawaamini kama Mpira umtinga nyavuni,Mtibwa wakiandika bao huku Yanga wakibaki wakilaumiana.

Golikipa wa Mtibwa akiwa haamini kunako dakika ya 85 ya mchezo pale Yanga waliposawazisha kupitia kwa Kiiza anaeshangilia huku akifuatiwa na Tegete katika mechi iliyoishia kwa Yanga 1-1 Mtibwa.
Picha na Bongo Staz Blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top