Kikosi cha Azama Fc kinachotarajiwa kushuka dimbani kesho katika mchezo wake na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom.
(Picha na Azam Fc)
Na Chediel Charles.
Azam Fc ambayo imefikisha pointi 33, sawa na Yanga inayoongoza ligi baada ya
kuifunga JKT Ruvu mabao 4-0 katika mchezo wa katikati ya wiki hii,kesho zinaingia katika mchezo baina yao unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Soka nchini.
Mpambano huo ambao unatabiriwa kuwa wa aina yake kutokana na ukweli kwamba mshindi wa mechi hiyo ataweza kuongoza ligi kwa kuwa na pointi 39.
Azam Fc imekuwa matokeo mazuri hivi karibuni kwa kushinda mechi nne mfululizo na kutoa ishara ya kuwa miongoni mwa timu zinazoleta changamoto kubwa kwenye soka hapa nchini.Hali iliyowalazimu wapinzani wao Yanga kuamua kujichimbia nje jiji ili kujiandaa na mechi hiyo ya kesho SOMA:YANGA YAINGIA KAMBINI ,hali hii imewashitua wapenda kandanda wengi kutokana na mazoea huko nyuma kwa timu kubwa kuingia kambini tu pale zinapopambana wao kwa wao(Simba na Yanga) na zinapocheza na timu ndogo huwa haziweki mkazo kama walivyoamua kwa Azam FC.
Mechi ya kesho ni muhimu kwa timu zote ili kuweza kupata pointi tatu muhimu lakini pia kuipa Azam Fc fursa ya kutoa changamoto kwa vilabu vikubwa hapa nchini ambavyo kwa miaka mingi vilionekana kuliteka soka kwa kupokezana Ubingwa wa Tanzania Bara.Kutetereka kwa Simba hakujaondoa ule msisimko kwani sasa Azam inaonyesha kutoa upinzani vilivyo kwa Yanga.
Je Azam 'wana lamba lamba' wataweza kuimudu Yanga kesho ? Dakika tisini kesho ndizo zitakazo amua nani atatoka na pointi tatu muhimu.
Post a Comment