Kikosi cha Young Africans Sports Club
.................
Timu ya Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligu Kuu ya
Vodacom nchini VPL kwa kuwa na point 36 na mabao 33 ya kufunga na mabao
12 ya kufungwa kesho itashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa kupambana
na timu ya waoka mikate ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya kuichapa timu
ya African Lyon katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa
mabao 4-0, watoto wa Jangwani watashuka dimba la uwanja wa Taifa kesho
kuhakikisha wanaondoka na point 3 muhimu na kuendeleza wimbi la ushindi
mfululizo katika mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom.
Kikosi
cha mholanzi Ernest Brandts kimeendelea na mazoezi leo asubuhi katika
uwanja wa mbegani pembeni kidogo ya mji wa Bagamoyo huku wachezaji wote
wakifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo utakaofanyika kesho
lakini pia wakionekana kuwa wenye morali ya hali ya juu dhidi ya mchezo
huo.
Kocha Mkuu Ernest mara baada ya mazoezi ya
leo asubuhi, amesema kikosi chake kipo tayari kabisa kuwavaa wauza lamba
lamba Azam FC siku ya kesho, na katika kambi yao ya siku tatu mjini
Bagamoyo imekua ni kambi nzuri na yenye maendeleo mazuri kwa wachezaji
wake wote na benchi la ufundi.
Azam FC najiua ni
timu nzuri, ina wachezaji wazuri lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya
kutuzuia sisi kuweza kuondoka na ushindi katika mchezo wa kesho, kwani
pamoja na kuwa wao wana timu nzuri ila sisi tuna nzuri na bora zaidi
kuliko timu yoyote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki 'alisema
Brandts'
Aidha
kocha Brandts amesema wachezaji wake wote 26 wako katika hali nzuri,
hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja katika kambi, na kesho atapata fursa
ya kumtumia mchezaji yoyote kati yao katika kuhakikisha anaibuka na
ushindi, kwani nimeiandaa timu yangu kuhakikisha inaondoka na poniti 3
katika mchezo huo.
Young Africana inahitaji
kushinda mchezo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya
kendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom ili mwishoni iweze
kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu 2012/2013.
Mungu Ibariki Young Africans , Mungu wabariki watoto wa Jangwani.
"YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
CHANZO:YANGA
Post a Comment