Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CHADEMA YAJIPANGA KUIBANA CCM ARUSHA


Kwa ufupi
“Tunataka uchaguzi mdogo ufanyike katika kata hizi kulingana na matakwa ya sheria. Tushinde Chadema, CCM, TLP, NCCR-Mageuzi au CUF sawa. Muhimu wananchi wapate haki ya uwakilishi kwenye vikao vya baraza la madiwani,” alisisitiza Mbowe.
...........
MWENYEKITI wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kusudio la chama chake kuanzisha ‘Libeneke’ alilosema Serikali itashindwa kulizima na kudai kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika kata tano za Jiji la Arusha zilizowazi kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Kata za Kimandolu, Themi, Kaloleni na Elerai ziko wazi tangu Agosti 7, mwaka juzi baada ya waliokuwa madiwani, Estomih Malla, Reuben Ngowi, Charles Mpanda na John Bayo na  wa viti maalum, Rehema Mohamed kufukuzwa uanachama wa Chadema kwa kosa la kukaidi maagizo ya kamati kuu kuhusu mwafaka wa mgogoro wa Umeya.
Kata ya Sombetini yenyewe iko wazi baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Alphonce Mawazo kuhamia Chadema akitoka CCM.
Mbowe alisema chama chake kitachukua mkondo wa shinikizo kwa Serikali na NEC baada ya kubaini mbinu za kuchelewesha makusudi uchaguzi katika kata hizo kwa kile kinachoaminiwa ni hofu ya CCM kuwa kata hizo zitatwaliwa na Chadema.
Akizungumza Arusha jana, wakati wa hafla fupi ya kupokea hati za kiwanja chenye ukubwa wa hekari tatu kutoka kwa Kampuni ya Mawala Trust kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maalumu ya Mama na Mtoto, Mbowe alisema wananchi wa kata hizo wana haki ya uwakilishi na Chadema itawasaidia kuidai.
Alisema chama chake pia kitaendesha kampeni ya kudai uchaguzi mdogo Sengerema na Buchosa alikosema pia kuna kata ziko wazi baada ya waliokuwa madiwani kupitia tiketi ya CCM kuhamia Chadema zaidi ya mwaka mmoja uliyopita.
“Tunataka uchaguzi mdogo ufanyike katika kata hizi kulingana na matakwa ya sheria. Tushinde Chadema, CCM, TLP, NCCR-Mageuzi au CUF sawa. Muhimu wananchi wapate haki ya uwakilishi kwenye vikao vya baraza la madiwani,” alisisitiza Mbowe.
Baada ya kuvuliwa uanachama, Mallah na wenzake wanne walifungua kesi kupinga uamuzi huo katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha, ambapo walishindwa na kukata rufaa Mahakama Kuu kabla ya kuamua kuifuta kwa hiari Septemba 5, mwaka huu.
Waliokuwa madiwani hao ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Severin Lawena, hivi sasa wameamriwa kuilipa Chadema fidia ya zaidi ya Sh15 milioni, baada ya Hakimu Mfawidhi, Charles Magessa kukubaliana na ombi la madai yaliyowasilishwa na Wakili Method Kimomogoro anayekiwakilisha Chadema na Mbowe aliyekuwa mdaiwa wa pili katika kesi ya msingi.

NA MWANANCHI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top