Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

GHOROFA YA 17 PPF TOWER YATEKETEA MOTO

 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU) akiangali Jengo la PPF Tower baada ya kuzima moto uliounguza sehemu ya  juu ya jengo hilo, jijinii  Dar es Salaam jana.
 Picha na Salhim Shao  
............
Kwa ufupi
Waandishi wa habari hizi  waliofika kwenye  jengo hilo  saa 3:00 asubuhi, walishuhudia moshi mkubwa ukifuka kutoka sehemu ya juu ya jengo hilo, ambako ipo mitambo ya mawasiliano na vifaa vingine.
.....................
SEHEMU ya jengo la kitega uchumi la Mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi (PPF) maarufu kama PPF Tower lililopo makutano ya barabara za Garden na Ohio,  Dar es Salaam limeteketea  kwa moto uliozuka ghorofa ya 17, alfajiri ya jana.
Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika, unadaiwa kuzuka katika ghorofa hiyo ambako kuna ofisi za Abbot Fund na Seven Seas.
Waandishi wa habari hizi  waliofika kwenye  jengo hilo  saa 3:00 asubuhi, walishuhudia moshi mkubwa ukifuka kutoka sehemu ya juu ya jengo hilo, ambako ipo mitambo ya mawasiliano na vifaa vingine.
Moshi huo ambao unadaiwa kuanza kuonekana tangu mapema alfajiri, uliendelea hadi muda huo na magari ya vikosi mbalimbali vya zimamoto yalifika eneo hilo na kuanza jitihada za kuzima moto huo. Magari hayo licha ya kupata maji kwa ajili ya kuzimia moto huo, kutokana na moshi uliokuwa umetanda katika jengo hilo kuanzia ghorofa ya 17 ulifanya washindwe kufika kwenye chanzo.
Waandishi walishuhudia watu watatu wakiwamo walinzi wa Kampuni ya KK Security wakiwa wamekwama sehemu ya juu ya jengo hilo, kutokana na ngazi za kushukia kukumbwa na moshi mzito.
Hata hivyo, saa 4:30 aubuhi baadhi ya askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiwamo wale wa kampuni binafsi waliweza kuwafikia watu hao na kuzima moto ambao ulikuwa unawaka eneo la juu la jengo.
Kaimu Kamishna wa Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto, Pius Nyambacha alisema walifika kwa wakati eneo la tukio na kwamba, miundombinu ya maji kwa ajili ya kuzimia moto iliyopo jengo hilo ilisaidia kufanikisha uzimaji huo.
Nyambacha alisema ni mapema kujua chanzo cha moto, lakini la msingi umethibitiwa na aliwataka wanaojenga majengo marefu kuzingantia uwekaji  miundombinu ya moto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik alisema miundombinu thabiti ya maji ya kuzimia moto katika jengo hilo, ndiyo iliyookoa  hasara zaidi.
“Wamejitahidi sana PPF kwani kila ghorofa lina miundombinu ya maji ya kuzimia moto, hali ambayo ilisaidia kuudhibiti,” alisema.

NA MWANANCHI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top