HABARI kutoka Jijini Mwanza kupitia G Sengo tunataarifiwa kuwa...
MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli
nchini(MSC)imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa
kampuni hiyo wakichomelea sehemu mojawapo ya Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji
la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC
yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika
kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zlizo patikana toka kwa wafanyakazi wa Meli
hiyo zimeleeza kuwa maundi wa kampuni walikuwa wakichomelea katika moja
ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto ulipoangukia
katika sehemu ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito
ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani
Kagera leo usiku.
Hata hivyo moto huo uliodumu kwa takribani nusu uliokuwa ukiwaka toka
katika chumba cha kuhifadhia mizigo kilichopo sehemu ya chini ya Meli
ya Mv Victoria ulidhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji
waliowasili katika eneo hilo mudamchache baada ya moto kuanza wakitumia
gari lenye namba z ausajili STK 1965 Mali ya Halmashauri ya jiji la
Mwanza.
Post a Comment