Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TMA:MVUA ITANYESHA CHINI YA KIWANGO

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeshauri mamlaka zinazohusika na nishati ya umeme kutumia njia mbadala katika uzalishaji kwa vile mvua inayotarajiwa kuanza kunyesha Machi hadi Mei, mwaka huu, itakuwa chini ya wastani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema matarajio ya mvua yatakuwa katika madaraja matatu ambayo ni juu ya wastani (asilimia 20), wastani (asilimia 45) na chini ya wastani (asilimia 35).

Vina vya maji katika maziwa, mabwawa na mito, havitarajiwi kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa kuwa mvua itakayonyesha msimu huu haitakuwa kubwa.

“Inashauriwa maji yatumike kwa uangalifu.

“Pia pamoja na matarajio ya mvua ya wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya nchi, uwezekano wa kutokea vipindi vya mvua kubwa hauwezi kuepukika.

“Hivyo, mamlaka za miji zinashauriwa kusafisha mifumo ya majitaka kuepusha maji kutuama na kupunguza madhara yatokanayo na mafuriko,” alisema.

Alisema sekta ya afya, inatakiwa kuchukua tahadhari ya maandalizi stahiki kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza ya milipuko ya magonjwa kama vile malaria, magonjwa ya macho na kipindupindu.

Alisema hali ya malisho na maji ya wanyamapori na mifugo, inatarajiwa kuwa nzuri katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua.

Maeneo mengi ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, nyanda za juu kaskazini mashariki, kanda ya Ziwa Victoria, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya kusini mwa nchi, yanatarajiwa kuwa na unyevunyevu wa kutosha wa udongo.

Alisema mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Dodoma, Singida, Lindi na Mtwara wakulima wanashauriwa kuendelea kufuata ushauri wa maofisa ugani na kutumia kwa manufaa kipindi cha mvua kilichobaki.

NA Mtanzania.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top