Bao lililofungwa na kiungo wa kimataifa raia wa Rwanda Haruna
Niyonzima dakika ya 66 ya mchezo, limeifanya timu ya Young Africans
kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini
Tanzania bada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo
uliofanyika leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa
Ligi Kuu ya Vodacom baada kufikisha point 42 na mabao 35 ya kufunga,
pointi 6 mbele ya timu inayoshika nafasi ya pili Azam Fc yenye pointi 36
huku timu zote zikiwa zimecheza michezo sawa.
Kikosi
cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika
15 za kwanza washambuliaji wake Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi
walikosa nafasi za wazi za kuweza kuipatia timu ya Yanga bao la mapema
kutokana na kupoteza nafasi za wazi.
Kagera Sugar ilicheza
soka la kushambulia kwa kushitukiza na kupitia washambuliaji wake Shija
Mkina na Darlington Enyima lakini umakini wa walinzi wa Yanga Kelvin
Yondani na Nadir Haroub 'Cannavaro' ulikuwa kikwazo kwao kuweza
kulifikia lango la watoto wa Jangwani.
Dakika ya 45 ya mchezo,
mwamuzi Simon Mberwa alitoa penati kwa Yanga kufuatia mlinda mlango wa
Kagera Sugar Hannington Kalyesubula kumchezea madhambi mshambuliji Dider
Kavumbagu, penati hiyo ilipigwa na Kavumbagu mwenyewe ambaye alikosa na
mpira kuwa wa kutoka.
Mpaka dakika 45 za kpindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo na kuhakikisha
wanasaka bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Kagera Sugar na
kuwachezea faulo nyingi washambuliaji wa Yanga ilipunguza radha ya
mchezo kutokana na mwamuzi kupuliza filimbi mara nyingi na kuharibu
mipango ya kupata bao.
Haruna
Niyonzima aliwainua washabiki wa Young Africans dakika ya 66 baada ya
kuifungia timu yake bao la kwanza na la ushindi baada ya kufanya
jitihada binafsi za kuwahadaa walinzi wa Kagera Sugar na kupiga shuti
kali ililokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa
Kagera Sugara akiruka kuuokoa mpira huo bila mafanikiko.
Kocha
Brandts alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Jerson Tegete na Hamis Kiiza
kuchukua nafasi za Said Bahanuzi na Didier Kavumbagu mabadiliko
yaliyoifanya Yanga kuendelea kuumiliki mpira na kucheza pasi za kuonana
kwa umakini zaidi, kwani kiungo FranK Domayo alipiga shuti kali
lililogonga mtambaa wa panya na kurudi ndani kabla ya kuokolewa na
walinzi wa Kagera Sugar.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1 - 0 Kagera Sugar
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kupata kwa
ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza washambuliaji hawakuwa
makini lakini kipindi cha pili timu ilibadilika sana hali iliyopelekea
kuutawala mchezo kwa kipindi chote na kupata bao hilo la ushindi
Kikubwa
tulikuwa tunahitaji ushindi wa pointi 3 amabzo tumefanikiwa kuzipata,
kila mchezo kwetu ni fainali ili kujiweka katika mazingira mazuri ya
kutwaa Ubingw, inabidi tushinde kila mchezo na ninashukru tumeshinda,
tunajiandaa na mchezo dhidi ya Toto Africans siku ya jumamos ya tarehe
09.03.2013 'alisema Brandts'
Baada
ya mchezo huu wa leo kikosi cha Young Africans kitaendelea na mazoezi
yake kesho asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama ikiwa ni
maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Toto African mwishoni
mwa wiki ijayo katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans:
1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twitel, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir
Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon
Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Said Bahanuzi/Jerson Tegete 10.Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima
Kagera Sugar:
1.Hannington Kalyesubula, 2.Benjamin Asukulie, 3.Muganyizi Martin,
4.Malegesi Mwanga, 5.Amandus Nesta, 6.Geroge Kavila, 7.Julius Mrope,
8.Juma Nade, 9.Darlington Enyima/Themi Felix, 10.Shija Mkina, 11.Daud
Jumanne/Paul Ngwai
Post a Comment