
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili
kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini
Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi
hizo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa ajili ziara
ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia
ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai
Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi
za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China,
Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini
China kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Ai
Ping, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China ( kulia) akiendesha
semina kwa kuhusu ujenzi wa vyama vingi katika mazingira ya utandawazi,
kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe
wake wa viongozi 14 wa CCM, leo Machi 19, 2013. Semina hiyo ilifanyika
katika Ofisi za Mambo ya Nje ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Viongozi wa CCM kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar),
Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed
Yusuf, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Katibu
Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.
Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa ajili
ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na ujumbe wake
wakiwa kwenye semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini
vijijini, semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa
cha kupambana na umasikini, Profesa Huang Chenwei (kushoto), katika
hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Wengine ni Katibu wa
NEC ya CCM, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(kulia), Kulia kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai
Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Yusuf na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu. Kinana na ujumbe
wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China kwa ajili ziara ya mafunzo,
kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na
Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakibadilishana mawazo,
baada ya semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini,
iliendeshwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha kupambana na
umasikini, Profesa Huang Chenwei, katika hoteli ya Wanshou, Beijing,
China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo
nchini China kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
Picha na Bashir Nkoromo
Post a Comment