 |
| Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John
Haule (kulia) kwa pamoja na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath
Shaw wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chuo
cha Diplomasia (CFR) cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India
(ICWA). Uwekaji saini huo ulifanyika Wizarani leo tarehe 19 Machi, 2013. |
 |
| Mkurugenzi
wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi (kushoto) pamoja na
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairukiwakishuhudia uwekaji
saini wa mkataba huo. |
 |
| Wajumbe
wengine waliohudhuria katika tukio hilo la uwekaji saini wa mkataba.
Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini, Bw. Gobal
Krisha na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria. |
 |
| Bw. Haule akibadilishana Mkataba na Balozi Shaw mara baada ya kusaini. |
 |
| Katibu Mkuu, Bw. Haule pamoja na Balozi Shaw wakionesha Mkataba huo. |
 |
| Katibu
Mkuu Bw. Haule akizungumza na Balozi Shaw mara baada ya kukamilisha
zoezi la uwekaji saini mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo cha
Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India. |
 |
| Mhe. Balozi Shaw akichangia hoja wakati wa mazungumzo na Bw. Haule huku wajumbe wengine wakisikiliza. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Tuesday, March 19, 2013
Post a Comment