Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, amefariki dunia jana (05.03.2013) baada
ya kuugua saratani na hivyo kufikisha ukingoni uongozi wake wa miaka
miwili katika taifa hilo la Amerika ya kusini lenye utajiri mkubwa wa
mafuta.
Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza leo kupitia kituo
cha televisheni nchini humo kuwa Chavez mwenye umri wa miaka 58 ameaga
dunia na kusema kifo chake kimewaacha na uchungu mwingi.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Chavez alishinda kirahisi muhula mwingine
wa miaka sita kuliongoza taifa hilo kwenye uchaguzi mkuu lakini
kutokana na kuzorota kwa afya yake, hakuweza kuhudhuria shughuli ya
kuapishwa kwake na hivyo kuilazimu mahakama ya juu nchini humo
kuahirisha shughuli hiyo kwa mda usiojulikana.
Kifo chake kimewahuzinisha mamilioni ya wafuasi wake waliopendezwa na
mtindo wake wa uongozi pamoja na sera zake kuhusiana na faida itokanayo
na mafuta ya taifa hilo yaliyowapunguzia pakubwa mzigo wa gharama ya
chakula na matibabu hasa kwa walioishi katika mitaa duni.
Kufuatia kifo cha rais huyo, makamu wake ametangaza kuwa wanajeshi na
polisi wamepelekwa kote nchini humo huku taifa hilo likiingia katika
kipindi kigumu cha kisiasa na maombolezo ili kulinda raia na kuhakikisha
kuna amani.
Post a Comment