|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akizungumza na Waziri wa Nchi wa Ireland anayeshughulikia masuala
ya Biashara na Maendeleo, Mhe. Joe Costello alipofika Wizarani kwa
mazungumzo na Mhe. Waziri Membe kuhusu kukuza ushirikiano kati ya nchi
hizi mbili na pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na
uwekezaji. |
|
Mhe.
Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha
ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi
Naimi Aziz (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. |
|
Mhe.
Membe katika mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha ni
ujumbe uliofuatana na Waziri huyo wa Ireland akiwemo Balozi wa Ireland
hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (wa kwanza kulia) |
|
Mhe. Costello akifafanua jambo kwa Mhe. Membe. |
|
Ujumbe wa Ireland wakati wa mazungumzo. |
|
Balozi
Msechu (kushoto), Balozi Naimi (katikati) pamoja na Bi. Zainabu Angovi
(kulia) wakisikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Costello
(hawapo pichani) |
|
Mhe. Membe akijadili jambo na Mhe. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland hapa nchini huku Mhe. Costello akisikiliza. |
|
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Costello mara baada ya mazungumzo yao. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Wednesday, March 13, 2013
Post a Comment