Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa
nyakati mbalimbali kati ya tarehe 28 Februari na 2 Machi 2013 kupitia
baadhi ya vyombo vya habari wametoa majibu yasiyokuwa ya kweli juu ya
mgawo wa dharura wa umeme uliotokea mwezi wa Februari.
Katibu
Mkuu wa Wizara Eliackim Maswi na Afisa Habari wa TANESCO Badra Masoud
wote wameeleza kwamba hakukuwa na mgawo wa umeme bali kilichotokea ni
matatizo madogo madogo ya mitambo na kwamba matengenezo yanaendelea.
Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ninazo taarifa
kwamba ukweli ni kuwa umetokea mgawo wa umeme wa dharura kutokana na
upungufu zaidi wa kina cha maji katika mabwawa ya kufua umeme, upungufu
wa fedha za kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kufua umeme
wa dharura na upungufu wa gesi asili ya kuendeshea mitambo ya kufua ya
umeme.
Hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kuingilia kati
kuwaeleza ukweli wananchi ikiwemo hatua zilizochukuliwa kuhakikisha
kwamba hali hiyo haiendelei mwezi Machi kinyume na ahadi iliyotolewa
bungeni tarehe 28 Julai 2012 kwamba mgawo wa umeme ungekuwa historia.
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Sunday, March 3, 2013
Post a Comment