Na Maggid Mjengwa,
JANA tulitafsiri maana ya ugaidi.
Tukangalia aina za ugaidi. Kisha tukaangaza kwenye chimbuko la ugaidi
duniani. Leo tutajadili juu ya chimbuko la ugaidi na kwa kutoa mifano,
tutaanza pia kuona mahusiano ya mwezi Septemba na vitendo vya kigaidi.

Wasalote
Kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kikundi cha Wayahudi kilipambana vikali
dhidi ya himaya ya Waroma katika iliyokuwa Palestina ya zamani. Kikundi
hiki kiliitwa Salote. Ni watu wenye hasira kali ikiwa na maana pia kuwa kilikuwa ni
kikundi cha kisiasa na kidini chenye imani kali. Kikundi hiki kilitaka
Wayahudi wote wazingatie yote kulingana na maagizo ya dini yao.

Wasalote walipambana kisiasa dhidi ya dola ya wavamizi ya Waroma.
Wasalote waliongozwa na Myahudi Galileo ambaye amri yake ya kuwataka
wafuasi wake kugoma kulipa kodi ndio ilikuwa chachu ya kuanzisha mapambano
ya kigaidi dhidi ya wavamizi wa Kiroma. Jambo hili linashuhudiwa pia katika
maandiko matakatifu ya Biblia juu ya kodi katika Agano Jipya.
Hatma ya Wayahudi haikujulikana , lakini, kiongozi mpya alijitokeza

na kuwaahidi Wayahudi ukombozi kutoka kwenye mikono ya wavamizi. Hatimaye,
baada ya machafuko yaliyodumu kwa miaka sabini, Wasolote waliangamizwa
baada ya Jerusalem kutekwa na hekalu kuangamizwa. Wasalote walirudi nyuma
hadi kwenye vilima vya Masada.
Baada ya kushindwa huko kwa Wasalote . Kikundi cha Wasalote wapatao elfu moja
walijiua kwa pamoja. Wasalote waliwaua kwanza wanawake , watoto na wazee,
baadae wanaume nao walijiua kabla ya Waroma hawajavitwaa vilima hivyo.
Inasadikiwa, kuwa tukio hili lilitokea mwaka 73 baada ya Yesu Kristo.
Wa-Assassine
Miaka elfu moja baadae lilijitokeza kundi jingine la kigaidi. Hawa waliitwa
Assassine. Waassasine walikuwa wafuasi wa dhehebu la dini ya Kiisamu lililokuwa
na makao yake makuu katika Iran ya leo. Kutoka huko Iran walimtuma kiongozi
wao aliyeitwa Hassan Ibn Sabah. Kwamba aende katika Mashariki ya Kati yote. Huko
akafanye mauaji ya kulipwa.
Wafuasi wa dhehebu hili walifahamika pia kwa kuvuta bangi kabla
hawajafanya tendo la kigaidi kwa jina la Mungu! Hapa tunaona neno
”Assassin”, kwa Kiingereza na hata kwa Kifaransa lina maana ya ”kuua” , yaani,
”Assasination” kwa Kiingereza, na kwa lugha ya Kiarabu linamaanisha ”
Mla-bangi”. Wa-assassin walikuwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia. Vitendo
vyao vya kigaidi viliwalenga zaidi Wasuni waliochukua sehemu kubwa ya
Persia.
Kunako mwaka 1200 vitendo vya kigaidi vya Wa-assasasine vilikoma. Ni
baada ya mjuukuu wa Djingis Khan kuangamiza ngome na makao makuu ya
Wa-assassine.
Utawala wa hofu 1773-94
Kwa kawaida, Mapinduzi ya Ufaransa uangaliwa kwa kutazama tarehe ile
Wafaransa walipovuka mstari wa Basti. Ni tarehe 14 Julai 1789. Kuna historia
yenye kuelezea tukio lile la kuvamia na kuvuka mstari ule. Kiuchumi, taifa la
Ufaransa lilikuwa katika wakati mgumu baada ya kushiriki vita kadhaa vyenye
gharama nyingi, na pia, hali ya ufalme wa nchi kutokulipa kodi ikiwemo kufanya
anasa ya kupindukia. Hali ya uchumi mbaya na mlipuko wa bei za bidhaa baada
ya vita vya gharama nyingi ndio iliyopelekea wananchi kuanzisha mapinduzi
yale.
Mfalme alikamatwa. Alifungwa gerezani baada ya jaribio lake la
kutoroka nchi kushindwa. Kati ya mwaka 1792 na Julai 1774, Ufaransa ilikuwa
chini ya himaya ya Maximilien Robespierre. Ulikuwa ni utawala dhalimu na
uliosambaza hofu kuu kwa watu wake, ” La Grande terreur” kwa lugha ya
Kifaransa. Lengo hasa la kusambaza hofu ile ilikuwa kuhakikisha mamlaka ya
Serikali ile ya kimapinduzi yanabaki chini ya walioshika himaya ya dola.
Kilikuwa ni kipindi ambacho, watu walikuwa na hofu hata ya kunong’ona
kuishutumu serikali. Watoa habari walikuwepo kila kona na hata ndani ya
familia. Inasadikiwa, kuwa Wafaransa takribani 40 000 walinyongwa bila hata
kufikishwa mahakamani. Kosa kubwa wakati huo ambalo mtu alihukumiwa
kunyongwa ni vitendo vyenye mwelekeo wa kupinga mapinduzi.
Magaidi wa Kiyahudi
Mwanzoni mwa miaka ya 1900, Mazayuni wa Kiyaudi walianzisha ujenzi wa
makazi ya Wayahaudi katika iliyokuwa Palestina ya zamani. Palestina
iliyokuwa chini ya himaya ya Osmani. Baada ya Vita Kuu ya kwanza, Palestina
ilikuwa chini ya udhamini wa Waingereza.
Baada ya kampeni ya vikundi vya kishawishi vya Wayahudi , Serikali ya
Uingereza ilitangaza kuwepo kwa taifa la Kiyahudi. Lakini, Serikali ya Uingereza ilionesha pia kutopendelea uwepo wa mradi ule wa ujenzi wa makazi ya Wayahudi.

Hali ile ilipelekea kuanzishwa kwa vikundi kadhaa vya kigaidi vya
Wayahudi vilivyopambana na Waingereza. Wakati wa Vita Kuu ya pili ya dunia , vingi ya vikundi hivi vilisimamisha harakati zao za kigaidi.
Baada ya Vita Kuu ya pili ya Dunia , vikundi hivyo vilianzisha tena
mashambulizi ya kigaidi kutetea kuwapo kwa taifa la Wayahudi . Moja ya
shambulizi la kigaidi la Wayahudi ni dhidi ya Hoteli ya Waingereza
iliyojulikana kama King David Hotel katika mji wa Jerusalem. Jengo la hoteli
liliangamizwa na watu 89 waliuawa.
Baada ya Vita Kuu ya pili ya Dunia, wahamiaji wengi zaidi wa Kiyahudi
waliendelea kuingia katika Palestina iliyokuwa katika udhamini wa
Waingereza. Lengo la kisiasa la Wayahudi la kuanzishwa kwa taifa la Uyahudi
lilipelekea kuanzishwa kwa vikundi zaidi vya kigaidi vyenye mitazamo ya
kitaifa. Viwili kati ya vikundi hivyo ni Irgun na Stern. Vikundi ambavyo vilitumia
mbinu za kigaidi katika kuendesha harakati zao. Miongoni mwa mbinu hizo ni
matumizi ya mabomu ya kutuma kwa barua.
Tangu mwezi Septemba 1947 hadi kutangazwa kwa taifa la Israel ,
mwezi Mei 1948, vikundi vya Irgun na Stern vilijulikana sana kwa matumizi
yake ya mabomu ya kutuma kwa barua.

Kabla na hata baada ya kutangazwa kwa taifa la Israel, vikundi vya Irgun na
Stern na baadae taifa la Israel, vimekuwa vikiendesha mashambulizi ya
kijeshi dhidi ya Wapalestina. Vitendo hivi viangaliwe hapa kama matendo ya
kigaidi dhidi ya watu wa Palestina , ambapo, lengo kuu ni kuwafukuza wale
wote wasio –Wayahudi. Ndipo hapa tunapoweza pia kubaini kiini cha mgogoro uliopo sasa kati ya Wapalestina na WaIsraeli.
Katika kufanakisha malengo haya, Israel imeendesha mashambulizi mengi
ya kigaidi katika vijiji na maeneo ya Waarabu. Takribani watu laki saba
walikimbia makazi yao katika vita vya awali kati ya Waarabu na Waisrael.
Watu hawa hawakuruhusiwa kurudi makwao. Hii ndio sababu, hadi hii leo, bado kuna Wapalestina wengi wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi, ndani ya ardhi yao, na hata katika nchi jirani kama vile Lebanon. Itaendelea...
0754 678 252

CHANZO: http://www.mjengwablog.com
Post a Comment