-
AWATISHA WAANDISHI KWA KUSEMA WANAZIWEKA ROHO ZAO REHANI.
-
MBUNGE WA MWIBARA (CCM) KANGI LUGOLA ASEMA KIONGOZI HUYO ANAUDHAIFU MKUBWA KIUONGOZI.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo akipokea heshima za gwaride
lililoandaliwa na kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo mkoani hapa.
Nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa
Polisi Liberatus Sabas na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo
(STPU) Tanzania Bara Kamishna Msaidizi wa Polisi Ibrahimu Kilongo.
(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Wakati CCM wakiendelea kumlalamikia Mkuu wa Mkoa (RC) wa
Arusha, Magessa Mulongo kwa hatua zake dhidi ya Lema, kiongozi huyo
jana aliwageukia waandishi wa habari wa Arusha akiwataka wawe makini
kipindi hiki, akidai kuwa nao wanatumika na wanasiasa.
Akihutubia katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi, alisema kuwa ikibainika wanatumika nao watafikishwa katika vyombo vya sheria.
“Mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, hivi hivi wakawa hawanielewi
na ikafika wakati wakanielewa kwani kuna miongoni mwao tulitaka
kuwafikisha katika sheria, lakini tukayaacha kwa kuwa sisi ndio walezi,”
alisema.
Mulongo aliongeza kuwa vitu ambavyo vinaandikwa si kweli kabisa, na
kwamba wataendelea kufuatilia kwani baadhi ya waandishi wanashirikiana
na wanasiasa kuwachafua viongozi wa serikali.
Alisema baadhi ya waandishi mkoani Arusha wamekuwa wakifanya kazi
zao kwa ushabiki wa kisiasa na kuandika mambo ambayo hawana uhakika
nayo.
“Unapoingia katika mkakati wa kudhalilisha kiongozi wa serikali unakuwa umeiweka roho yako rehani, kuweni makini,” alisema.
Aidha alivionya vyama vya wafanyakazi mkoani Arusha kutoruhusu
kutumiwa na watu kwa malengo ya kisiasa na pia waajiri waache kufanya
kazi bila kufuata taratibu na sheria.
Hatua hiyo imeendeleza mpasuko ndani ya chama cha CCM wakiwemo
wabunge, na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi
alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
(CHADEMA).
Wabunge hao walinukuliwa wakisema
kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa
shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola
alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye
kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka za utendaji
kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi
CHADEMA.
“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini
ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu
Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka,
utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema
aonekane shujaa.
“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo
wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya
ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema
Lugola.
Mbunge mwingine ambaye aliomba jina
lake lihifadhiwe, alisema alichokifanya Mulongo ni sehemu ya tatizo
kubwa la viongozi wa serikali kujihusisha na ukereketwa wa kisiasa.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi, tena hakumtaja jina, kwamba anapendwa
kubebwa, alisema mwacheni abebwe. Alisema vile kuwazuia polisi
kukabiliana na watu wanaopenda kumbeba kiongozi huyo.
“Mkuu wa Mkoa Arusha na wengine
wanaokabiliana na wapinzani kwa nguvu kubwa bila sababu, hii
inawaongezea umaarufu,” alisema mbunge huyo kutoka moja ya majimbo ya
kanda ya kati.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya
CCM ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alilaani jinsi mkuu wa mkoa
huyo alivyojikoroga katika kushughulikia mzozo wa Chuo cha Uhasibu
Arusha.
“Niliposoma ujumbe wa simu ya
mkononi wa Lema ambao alidai umetoka kwa Mkuu wa Mkoa, nilishangaa sana.
Sijui kwanini amefanya vile,” alisema kigogo huyo.
Aprili 24 mwaka huu, Mulongo
aliliamuru Jeshi la Polisi mkoani Arusha kumkamata Lema kwa madai kuwa
aliwachochea wanafunzi wa chuo hicho cha IAA kumzomea na kumrushia
mawe.
Lema alizingirwa nyumbani kwake na
maofisa wa polisi kitengo cha upelelezi na wale wa doria Ijumaa saa 5.30
usiku kisha kuchukuliwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuwekwa
rumande siku tatu hadi Jumatatu wiki hii alipofikishwa mahakamani.
Hata hivyo, madai ya Mulongo kuwa
Lema alichochea wanafuzni hao yanakinzana na ushahidi wa video
unaoonesha kuwa mbunge huyo alitumia kila aina ya ushawishi kuwasihi
wasiandamane kufuatia mwenzao Elly Kago (22) kuuawa na watu
wasiojulikana jirani na chuo.
Mapema kabla ya kukamatwa, Lema
aliitisha mkutano na waandishi wa habari akidai kutishiwa na Mulongo
kupitia ujumbe wa maandishi wa simu.
“Umeruka kihunzi cha kwanza,
nitakuonyesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa
kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu
namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Thursday, May 2, 2013
Post a Comment