  | 
| Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe 
(Mb.) (katikati) akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa 
nchini (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kitaifa.
 Katika Mkutano huo Mhe. Membe alifafanua juu ya hali ya kisiasa nchini 
Madagascar na Zimbabwe na kutoa taarifa za kuwasili kwa vikosi vya 
kulinda amani vya Tanzania huko Mashariki mwa DRC. Kuhusu masuala ya 
kitaifa Mhe. Membe alilitolea ufafanuzi suala la shambulio la bomu 
lilitokea hivi karibuni huko Arusha ambapo alisema kuwa Serikali 
inaendelea na uchunguzi  na kwa ujumla hali nchini ni tulivu. Wengine 
katika picha ni Bw. John Haule (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
 ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe.Khalfan  Juma Mpango (kulia),
 Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa 
nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es 
Salaam tarehe 13 Mei, 2013. | 
  | 
| Baadhi
 ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakurugenzi wa 
Idara mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 
Kimataifa  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) | 
  | 
| Mabalozi wengine wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) | 
  | 
| Naibu
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
Balozi Rajab Gamaha (wa pili kushoto) kwa pamoja na baadhi ya Mabalozi 
wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza mhe. Waziri Membe 
(hayupo pichani) wakati alipozungumza na Mabalozi hao. | 
  | 
| Mabalozi wengine na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) | 
  | 
| Sehemu nyingine ya Mabalozi wakati Mhe. Membe alipozungumza nao. | 
  | 
| Mkurugenzi
 na Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 
Kimataifa, Balozi Mohammed Maharage (kushoto) akimsikiliza Mhe. Waziri 
(hayupo pichani) alipozungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa 
nchini. | 
  | 
| Balozi Mpango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake mara baada ya Mhe. Membe kumaliza mazungumzo nao. | 
  | 
| Picha zaidi za mkutano huo wa Mhe. Membe na Mabalozi. | 
  | 
| Mhe. Membe akiagana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Sebregondi mara baada ya mazungumzo na Mabalozi hao. | 
  | 
| Mhe.
 Waziri Membe akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),
 Mhe. Balozi Abdulla Ibrahim Al-Sowaidi hapa nchini baada ya kumaliza 
mazungumzo. | 
  | 
| Mhe.
 Membe akiteta jambo na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa 
nchini, Mhe. Francisco Montecillo Padilla mara baada ya kuzungumza na 
Mabalozi hao. | 
  | 
| Mhe. Membe akiasalimiana na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Alfonso Lenhardt aliyekuwepo wakati wa mkutano huo. | 
  | 
| Balozi wa Rwanda hapa nchini akifuatana na Mhe. Membe alipomaliza mazungumzo na Mabalozi hao. | 
  | 
| Mhe.
 Membe akizungumza na Waandishii wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya 
mazungumzo yake  na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hao hapa nchini. | 
 
 
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
 
Filed Under: 
          
Jamii
  on Tuesday, May 14, 2013
 
 
Post a Comment