Kwa ufupi
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama
anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu
Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson
Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Benjamin Mkapa.
...........
Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga
kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu
kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza
uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu
Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa
na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha
Rose Migiro.
“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu
anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili
kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa
mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias
Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais
wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za
heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka
Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini
Uingereza,David Mellor.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI

Post a Comment