Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akiingia bungeni Dodoma jana kusoma hotuba ya Bajeti. Picha na Fidelis Felix.
Kwa ufupi
.........
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, viwango
vinavyopendekezwa ni ikiwa mfanyakazi anapata jumla ya mapato yasiyozidi
Sh2,040,000 kwa mwaka ambayo ni sawa na Sh170,000 kwa mwezi, kiwango
cha kodi ni asilimia 0, kwa maana kwamba hatalipa kodi.
,,,,,,,,
Dar es Salaam. Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14 inaonyesha
kuwa wafanyakazi wamepunguziwa kodi katika mishahara yao ingawa punguzo
lenyewe linaonekana kama kiini macho.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Serikali bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, William Mgimwa alisema
Serikali imependekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato
ili kupunguza kodi hiyo.
Waziri Mgimwa alisema Serikali imepunguza kiwango
cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi
13... “Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi.”
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, viwango
vinavyopendekezwa ni ikiwa mfanyakazi anapata jumla ya mapato yasiyozidi
Sh2,040,000 kwa mwaka ambayo ni sawa na Sh170,000 kwa mwezi, kiwango
cha kodi ni asilimia 0, kwa maana kwamba hatalipa kodi.
Kwa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi
Sh2,040,000 lakini hayazidi Sh4,320,000 sawa na Sh360,000 kwa mwezi
kiwango cha kodi atakachokatwa ni asilimia 13 baada ya malipo ya Mfuko
wa Jamii ambayo ni nafuu ya isiyozidi Sh1,540.
Kwa wafanyakazi wenye mapato yanayozidi Sh361,000 kuendelea watapata nafuu ya Sh1,900.
MISHAHARA KIMYA
Dk Mgimwa hakuzungumzia suala lolote kuhusu
kupandishwa kwa mishahara tofauti na kilio cha Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (Tucta), ambalo katika sherehe za Mei Mosi, mwaka huu
zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya, lilipendekeza kima cha chini cha
mshahara kiwe Sh740,000 kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
MWANANCHI
MWANANCHI

Post a Comment