Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika
*Mnyika: Watuhumiwa wa tindikali wanateswa kwa umeme
*Asema CCM inaandaa mashitaka kwa Mbowe, Lissu, Slaa
*Nape ampa siku tatu kutoa ushahidi, vinginevyo atamuumbua
*Polisi wasema hawaangalii rangi ya mtu, wanafuata sheria
VITA ya maneno ya kutuhumiana baina ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Mapinduzi (CCM) na makamanda wa juu wa Jeshi la Polisi, sasa imeanza kuchukua sura mpya kwa kila upande kutishia kutoa ushahidi kwa wananchi unaoonyesha jinsi unavyohujumiwa na upande mwingine.
Madai haya yamekuja huku fukuto la vita ya maneno baina ya CCM, Chadema na Polisi kuhusu chanzo na wahusika wa mlipuko wa Bomu katika mkutano wa lala salama wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Chadema, uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya Soweto, Arusha likiwa bado halijapoa.
Tangu kutokea kwa mlipuko huo wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 70, viongozi wakuu wa Chadema wamekuwa wakidai kuwa Polisi ndiyo waliohusika, huku CCM kikiituhumu Chadema kuhusika na unyama huo.
Kutuhumiana huko kukiwa kunaendelea, jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alikutana na waandishi wa Habari makao makuu ya chama hicho, Dar es Salaam na kuibua tuhuma mpya dhidi ya viongozi wa CCM na baadhi ya makamanda wa ngazi za juu wa Polisi.
Katika mkutano huo, Mnyika alieleza kuwa chama chake kimenasa nyaraka za uhakika kutoka kwa watu walio ndani ya CCM na Polisi, zinazowaonyesha viongozi wa CCM na makamanda wa polisi wakipanga njama za kuwamaliza kisiasa viongozi watano wa Chadema.
Muda mfupi baada ya Mnyika kuibua tuhuma hizo, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliliambia Mtanzania kupitia simu yake ya kiganjani kuwa anakitaka Chadema kutoa ushahidi wa tuhuma hizo katika muda usiozidi siku tatu, vinginevyo yeye atajitokeza na kueleza jinsi ambavyo kimekuwa kikijihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Katika maelezo yake Mnyika, aliwataja viongozi wa kitaifa wa chama hicho wanaoandaliwa mipango ya kubambikiwa kesi kuwa ni Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa), Dk. Wilbrod Slaa (Katibu Mkuu), Tundu Lissu (Mbunge na Mwanasheria), pamoja na yeye mwenyewe Mnyika.
Aliwataja baadhi ya watu wanaotajwa katika ushahidi wa maandishi na ule wa mkanda wa video kuhusika katika mipango hiyo kuwa ofisa wa juu wa Polisi aliye makao makuu, Advocate Nyombi na Naibu Katibu Mkuu Bara CCM, Mwigulu Nchemba.
Mnyika alisema tayari polisi wamekwishaanza kutekeleza mpango wa kuwahujumu viongozi wa chama hicho kwa kumkamata Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Hanry Kileo, kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kummwangia tindikali kada wa CCM, Mussa Tesha, wakati wa Uchaguzi mdogo wa Igunga mwaka 2011.
“Kuna viongozi wetu wamekamatwa na kuunganishwa katika kesi dhidi ya kada wa CCM aliyemwagiwa tindikali kule Igunga. Lakini mbali ya hilo kuna njama za polisi na viongozi wa chama tawala kufanya vikao vya kupanga kuwaangamiza viongozi wa Chadema ngazi ya taifa, kwa kuwapa kesi zisizo za kweli.
“Hadi sasa wanachama watano wa Chadema wamekamatwa na kuteswa kwa kupigwa wakilazimishwa kukubali kuhusika katika tukio la kumwagiwa tindikali kada wa CCM, huku wakiwataka kuandika maelezo kwamba waliagizwa na viongozi wetu wa kitaifa,” alisema Mnyika.
Katika kuthibitisha madai yake, Mnyika alisema Chadema kinao ushahidi wa mkanda wa video unaoonyesha jinsi wanachama wao walivyokuwa wakiteswa na polisi kwa kulazimishwa kuweka saini maelezo yaliyokuwa yameandikwa na polisi na walipokataa waliteswa kwa kuwekwa katika nyaya za umeme.
“Makada wetu waliokamatwa hadi sasa ni watano ambao ni Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta, Rajabu Kihawa na Hanry Kileo ambao kwa pamoja wamehusishwa na kesi ya tindikali, huku wakiwalazimisha kukubali kuwa waliagizwa na viongozi wa kitaifa.
“Pia makada hao wanalazimishwa kukubaliwa kuwa walionunua tindikali hiyo na kuwapatia utekelezaji ni John Heche, Wilfred Lwakatare na Ahmed Sabula ambao wote ni viongozi wa Chadema katika ngazi mbalimbali,” alisema Mnyika.
Akizungumzia mipango ya kubambikia kesi viongozi wa Chadema, alisema Chadema kimekamata nyaraka za uhakika ambazo kiko tayari kuzitoa kwenye vyombo vya sheria kama ushahidi zinazoonyesha jinsi vikao vilivyokuwa vikikaa kati ya maofisa wa jeshi la polisi na baadhi ya viongozi wa CCM.
Alikishutumu CCM kuwa kimefilisika kisera na hoja kiasi cha kuamua kutembea na kijana aliyemwagiwa tindikali, huku kikieneza uongo kuwa Chadema ni chama cha magaidi.
Aliwataka Watanzania kujiuliza idadi ya vijana wa Chadema na wananchi wa kawaida waliouawa katika mikutano ya siasa na wengine kuvamiwa nyumbani, huku polisi wakishindwa kuwakamata wahusika wanaotajwa moja kwa moja na matukio hayo ambao ni makada wa CCM.
“Tunapenda kusisitiza kwamba Chadema katika kueneza sera sahihi, kuleta uongozi bora, mikakati makini na oganaizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania, tutaendelea kusonga mbele kwa sababu ya nguvu ya umma inayosukuma kasi kubwa ya mabadiliko nchini,” alisisitiza Mnyika.
Akieleza mikakati ya chama hicho kuwanusuru makada wake wanaokabiliwa na kesi ya tindikali, alisema Chadema kimeteua mawakili saba watakaokuwa wakisimamia kesi za wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wao.
Alimtaja Profesa Abdallah Safari kuwa ataongoza jopo la mawakili wanne wa chama hicho kuwatetea wanachama na viongozi wa Chadema katika kesi mbalimbali zinazowakabili mahakamani.
Profesa Safari ambaye alipata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo, alisema njama zinazofanywa dhidi ya Chadema hazitafanikiwa kwa sababu chama kimejipanga vizuri kuzikabili.
Alisema kesi ya tindikali, Serikali pamoja na CCM watarajie kushindwa kwa sababu mawakili wa Chadema wamejipanga kuhakikisha ukweli unakuwa wazi, ili Watanzania wafanye uamuzi sahihi.

CCM yajibu mapigo
Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu tuhuma hizo, Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM, Nape Nnauye, aliitaka Chadema kutoa ushahidi unaowahusisha viongozi wake na makamanda wa juu wa polisi na mipango ya kukihujumu ndani ya siku tatu na isipofanya hivyo atajitokeza na kuueleza umma ushahidi alionao kuhusu tukio la kada wa CCM kumwagiwa tindikali huko Igunga.
“Ninawataka Chadema wajitokeze hadharani ndani ya siku tatu na watoe ushahidi wao. Na wasipofanya hivyo nitajitokeza mbele ya umma wa Watanzania kueleza ushahidi wa tukio hilo.
“CCM inapenda kuwaambia Chadema wasitumie kivuli cha umma kutaka kuficha maovu yao na kama wao wapo tayari ninawataka wajitokeze na watoe ushahidi wao,” alisema Nape.

Jeshi la Polisi laibuka
Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema jeshi hilo linafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wake.
“Katika utendaji wa Jeshi la Polisi na utaratibu wake wa kuzuia na kukabiliana na uhalifu, haliangalii chama cha mtu, kabila wala rangi,” alisema Senso.

MTANZANIA
Post a Comment