Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
.......
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa
jambo lolote linalohusu uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika
Jumapili wiki iliyopita, jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa
huo.
Alisema hayo alipozungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne.
“Waulize wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua chama chetu kimegawa majukumu. Kule kuna mwenyekiti wa mkoa, katibu pamoja na wengineo,” alisema Nape.
Alipoulizwa sababu za kutoa maoni katika chaguzi nyingine mara tu matokeo yanapotangazwa, kama vile Jimbo la Igunga, Nape alisema uchaguzi huo unahusu ubunge tofauti na udiwani.
Alisema hata katika uchaguzi wa kata nyingine 22, alizungumza kwa kuwa ulikuwa umehusisha kata mbalimbali nchini na siyo mkoa mmoja.

CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment