Kikosi
kazi cha Skylight Band kwenye picha ya pamoja ndani ya uwanja wa Ngome
Kongwe visiwani Zanzibar walipopata mwaliko kutumbuiza kwenye tamasha la
ZIFF 2013 kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa Band hiyo ambayo
haijamaliza hata mwaka.
Kikundi
cha ngoma za Asili inayofahamika kama "KIDUMBAKI" kikitoa burudani
kwenye tamasha za ZIFF linaloendelea Visiwani humo eneo la Ngome Kongwe.
Mmoja
wa Wanenguaji wa Ngoma ya asili ya KIDUMBAKI akionyesha ufundi wake wa
kunyonga kiuno ambapo alionekana kuvutia wengi na kucheza vizuri
kushinda kinadada....Mambo ya Pwani hayo aatiiiiiiiiii.
Wanamuziki
wa Skylight Band wakishambulia jukwaa wakati wa tamasha la Zanzibar
International Film Festival 2013 (ZIFF) linaloendelea kwenye viwanja
vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
Aneth
Kushaba AK 47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight
Band kwenye uwanja wa Ngome Kongwe Visiwani Zanzibar wakati wa tamashala
ZIFF 2013.
Baadhi ya raia wa kigeni wakijaribu kucheza style mbali mbali za Band hiyo kwenye tamasha la ZIFF 2013.
Sam
Mapenzi akiongozi wasanii wenzake kutoa burudani kwa Wanzibari na
wageni kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria tamasha la ZIFF 2013
usiku wa kuamkia leo ambalo linaendelea kwenye uwanja wa Ngome Kongwe.
Baadhi
ya raia wa kigeni wakilisakata Sebene lililokuwa likiporomoshwa na
Skylight Band kwenye tamasha la ZIFF 2013 visiwani Zanzibar
Binti mwenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni Mary Lukas akiwapa raha mashabiki wa tamasha la ZIFF 2013 visiwani Zanzibar.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa Bongo kutoka Skylight Band akishindani na kijana Kassim kulisakata sebene.
Mpiga
Drum mahiri wa Skylight Band Idrisa akiwa kibaruani kuhakikisha
mashabiki wa Band hiyo wanapata ile ladha halisi. Njoo Thai Village
Ijumaa hii ushuhudie maufundi ya kijana huyu.
Mmoja
wa wa watoto aliyeonekana kuwa kivutio kwa wengi akishindina kusakata
sebene na raia wa kigeni wakati wa tamasha la ZIFF 2013.
Wageni walichizika kushinda hata wenyeji kama inavyoonekana pichani.
Full kujiachia na kwaito ilichezeka. Hapana chezea Skylight Band weweeeeeee.!
Umati
wa wageni kutoka mataifa mbalimbali uliofika kushuhudia show ya kukata
na shoka iliyopigwa na Skylight Band usiku wa kuamkia leo Ngome Kongwe
visiwani Zanzibar.
Mary Lukas akishow love na Mpiga Bass Guitar Chilichala back stage wakati wa tamasha la ZIFF 2013.
Post a Comment