Mke wa Rais wa Markani mama Michelle
Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA jioni
hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na
mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu
ya taaisis hiyo leo, Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako
katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana na
watoto wao jioni hii Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji
wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari
Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.
Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete
Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF
akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack
Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii
Picha na http://www.fullshangweblog.com/
Post a Comment