Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TCU YAFAFANUA SHULE KUKOSA WA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO


Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imesema hakutakuwa na uhaba wa wanafunzi vyuo vikuu licha ya shule za serikali kukosa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa TCU, Edward Mkaku, alipozungumza na NIPASHE ofisini kwake.

Mkaku alisema kuwa mtu kama amefeli kidato cha nne, atalazimika kurudia na hapaswi kukata tamaa.

Mkaku alisema hakuna haja ya wanafunzi waliofeli kidato cha nne kukimbilia kidato cha tano ama chuo, kwani hakuna chuo kinachokosa wanafunzi kila mwaka na wala vyuo havina kazi ya kufundisha pekee bali ina kazi tatu za kufanya zikiwamo za utafiti, kufundisha na kutoa ushauri wa kiufundi au kitaalam.

Alifafanua kwamba wapo wanafunzi wengi wanaoweza kuingia vyuo vikuu wakiwamo wanaosoma ngazi ya cheti, stashahada na siyo lazima wawe wamehitimu kidato cha sita.

Kauli ya TCU inafuatia wanafunzi 10,000 kukosa nafasi za shule kidato cha tano kutokana na kukosa sifa.

 
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top