Mratibu wa mipango ya maendeleo ambaye pia ni diwani katika manispaa ya 
Arvidsjaur,Stina Johansson(tatu Kulia) akiwa na ujumbe wa viongozi 
kutoka wilayani Hai-kutoka kulia,Novats Makunga(Mkuu wa wilaya),Clement 
Kwayu(Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya),Melkizedeck Humbe(Mkurugenzi 
Mtendaji wa Halmashauri) na Ester Mbatiani ambaye ni afisa mipango mkuu 
wa Halmashauri
 Watendaji wa Manispaa ya Arvidsjaur na halmashauri ya wilaya ya Hai wakibadilishana mkataba wa ushirikiano
 Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na wale wa Manispaa ya Arvidsjaur katika kusainiana makubaliano ya ushirikiano
Meya wa manispaa ya Arvidsjaur,Jerry Johqnsson(Katikati) akifafanua 
jambo baada ya kumalizika itifika ya kusaini makubaliano na hamashauri 
ya wilaya ya Hai,anayeshuhudia ni mwenyekiti wa halmashauri Clement 
Kwayu
Na Richard Mwangulube,Hai
Na Richard Mwangulube,Hai
Halmashauri ya wilaya ya Hai,imeingia mkataba wa miaka minne wa ushirikiano na Manispaa ya Arvidsjaur  nchini  Sweden  unaolenga katika maeneo ya kiuchumi na kijamii
ukiwemo wa teknolojia ya kisasa ya udhibiti wa takataka kiuchumi kwa
kuziwezesha kutengezwa upya bidhaa kwa ajili ya matumizi
Mkataba huo
ulitiwa saini  wakati wa ziara ya ujumbe wa viongozi  wa wilaya
ya  Hai uliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya
Hiyo, Novatus Makunga hivi karibuni katika  makao Makuu ya Manispaa hiyo nchini Sweden.
Wajumbe wengine
Katika ziara hiyo ya siku tano ambao ndiyo waliosaini mkataba huo ni pamoja na Mwenyekiti
wa Halmashauri  ya Wilaya ya Hai Clement Kwayu, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Melkizedeck Humbe pamoja na Afisa Mipango   wa
Halmashauri Ester Mbatian
Kufuatia
 mkataba huo, Halmashauri ya Wilaya ya Hai itapaswa  kuandaa na
kuwasilisha katika Manispaa ya Arvidsjaur  miradi mbalimbali inayolenga
katika Nyanja za biashara na  viwanda vidogo na vya kati
Maeneo mengine
ya shirikiano huo ni pamoja na  elimu na
utoaji wa taarifa, uboreshaji   na usimamizi  wa mazingira
endelevu pamoja na miradi inayolenga   masuala ya  ajira 
kwa vijana.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Hai mwishoni mwa wiki,Makunga  amesema kadhalika
ushirikiano ho unalenga  katika kuimarisha 
shughuli  mbalimbali zinazohusiana na masuala ya sekta ya utalii na utawala
bora kuanzia ngazi ya chini kabisa.
“Kwa
kushirikiana na wenzetu tunaandaa mkakati wa kuimarisha mafunzo kwa  jamii
katika masuala ya uchumi na  shughuli za maendeleo ya Kijamii na lengo kubwa
zaidi ni kwa kundi la vijana”. Amefafanua Makunga
Ameeleza kupitia
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden[SIDA] ushirikiano huo pia   utatoa
fursa kwa Manispaa ya Arvidsjaur kushirikiana na wilaya ya Hai katika ujenga
uwezo kwa halmashauri juu ya namna ya kupata taarifa mbalmbali za
maendeleo  na kiuchumi kutoka maeneo ya vijijini nakuzifanyia kazi. 
Amesema pia
ushirikiano huo umelenga katika kuhakikisha halmashauri ya Hai inaingia katika
mfumo wa kisasa wa namna ya kusimamia  ukusanyaji wa mapato na matumizi ya
fedha za maendeleo, kuboresha mawasiliano na wadau mbalimbali  ikiwemo kupitia kituo cha halmashauri hiyo cha
redio  Boma FM
Amesemasa Manispaa 
hiyo ya Sweden  itasaidia  katika
ujenzi,uboreshaji na uendelezaji wa  kituo cha  mafunzo kwa ajili
ya  maendeleo ya jamii katika wilayani Hai pamoja na kusaidia  katika
kuboresha huduma za afya
Masuala mengine
yatakayotekelezwa  kutokana na mahusiano hayo  ni pamoja na Manispaa ya Arvidsjaur kusaidia
katika teknolojia ya urudufishaji wa taka ambapo unawezesha taka ngumu na taka
maji kuweza kutumika tena.
Makunga amesema
kuwa suala la udhibiti wa takataka ni changamoto kubwa katika mji wa Hai ambao
hauna dampo huku kukabiliwa na ongezeko la kasi la watu wanaopenda kuweka makazi
ya kuishi na kuendesha shughuli zao za kazi Arusha,Moshi,Siha na Simanjiro.
“Kwa wenzetu taka ni rasilimali,
inachambuliwa kuanzia ngazi ya familia na kupelekwa eneo la kutupa taka, kwa
kupangwa kuangalia na aina, na hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali vikiwemo
vikombe, vijiko, sahani na umeme pamoja na mafuta ya kulainishia vyuma kutumika
upya,”amefafanua
Ametaja mengine
ambayo yatatiliwa mkazo kutokana na ushirikiano huo ni pamoja na  Manispaa
hiyo kusaidia katika kukuza uchumi na kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi.
Makunga ameeleza
kuwa manispaa hiyo ambayo inamiliki uwanja wa ndege wa kimataifa imeonyesha
kuvutiwa kusaidia uimarishaji wa  uwanja
wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)  uliopo
wilayani Hai kwa kuongeza  shughuli za  biashara za Anga pamoja na
kuboresha miundo mbinu katika Uwanja huo
Ujumbe huo
uliweza kupata taarifa juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Manispaa
hiyo zikiwemo za kuchumi, kijamii pamoja na usimamizi bora  wa ukusanyaji
na matumizi ya Mapato
Kwa mujibu wa nchi
ya Sweden, Mamlaka zote  za Serikali za Mitaa zinajulikana kama
Manispaa zinaongozwa kwa sheria ya bunge la nchi hiyo ambapo hivi sasa kuna
Manispaa zipatazo 260 nchini Sweden
Manispaa hizi zinawajib
wa kusimamia  masuala ya  elimu kuanzia ngazi ya chekechea hadi
Sekondari pamoja na kujenga na kusimamia vituo vya malezi ya  wazee na
wasiojiweza
Kadhalika manispaa
hizi zinawajibu wa  kusimamia vituo vya zimamoto na uokoaji,kusimamia
ujenzi  na uendeshaji  wa viwanja vya ndege,kusaidia walemavu pamoja
na kuunganisha wajiri na waajiriwa
Pia Makunga ameeleza kuwa Manispaa hizi zinajukumu la kusimamia vituo vya elimu ya ujasirimali kwa vijana na masuala ya Utalii ambapo Sweden kila siku hupokea watalii zaidiya 500,000 wanaotembelea vivutio mbalimbali katika Manispaa hizo kutoka nchi za ulaya
     CHANZO:BOMA BLOG                                                                                                                                                                                                                            

Post a Comment