Shabiki wa Simba akidhibitiwa na Polisi alipokaidi amri ya kuondoka pale mashabiki wa Simba walipoanza kung'oa viti katika Uwanja wa Taifa baada ya kukasirishwa na matokeo ya sare kati aya Simba na Kagera Sugar.
Alipoona virungu vinazidi aliamua kuruka kutoka jukwaani hadi chini ambapo alipokelewa juu kwa juu
Mara baada ya kutua akajikuta chini ya ulinzi wa Polisi waliokuwa wanamsubiri kwa hamu
Hapo akiwa amedhibitiwa vilivyo
Huku akijitahidi kutoa maelezo lakini hakuna aliyekuwa akimsikiliza Hakuna kutoka hapa wanaita Tanganyika jeki
Picha kwa hisani kubwa ya blog ya Habari Mseto,audifacejackson.blogspot.com