Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA:RAIS KIKWETE AKIWA NA NAIBU WA RAIS WA KENYA MHE.RUTO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete ambaye alitua nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo. 
PICHA NA IKULU
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top