Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI WA FEDHA AKIRI HALI NGUMU

 
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya  
,,,,,,
Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo.
Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi Jumapili kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.
“Ni kweli nimesikia alichosema CAG na nadhani alimaanisha kudhibiti matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji. Siyo kwa Tanzania tu, nchi zote huwa zinazingatia matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji yaliyopo” alisema Saada na kuongeza:
“Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo.”
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na ofisi yake kufanyiwa kazi.
CHANZO:MWANANCHI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top