Kutoka
Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa
na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema
zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.
Miongoni mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga
Omary Nundu,gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar
na Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka
yaliporwa na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema David Misime amesema Mpaka sasa jeshi
la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya
kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo inasema vijana zaidi ya 300
wakishirikiana na wabeba mizigo wa Kibaigwa walifanya maandamano yasiyo
na kibali na kung’oa bango la halmashauri ya kongwa lililokua na tangazo
la kukataza wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru.
Baada ya bango hilo vijana hao waliamua kufunga barabara kuu ya
Dodoma Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi baadae walivamia maduka na
kupora vinywaji na kuvunja majokofu.
Chanzo cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao Kibaigwa
kupinga kitendo cha Halmashauri ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza
ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba inawakosesha kufanya kazi zao
kwani wateja wao wanashindwa kuingiza mazao sokoni.
Post a Comment