Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA:NAIBU WAZIRI WA MAJI ,AMOS MAKALLA AKAGUA MAENDELEO YA UPANUZI WA MITAMBO YA MAJI WA RUVU JUU,MKOANI PWANI


Meneja Mkuu wa Kampuni ya ufyatuaji matofali ya Ujenzi Solutions, ya Kimara kwa Msuguri, Dar es Salaam, Rahim Hamis na mfanyabiashara wa kampuni isiyo na jina, Credo Rajab (kulia) wakiwa chini ya uliznzi wa Polisi huku wakiwa wamevishwa pingu baada Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kuamuru kuwakamata alipokagua viwanda vyao vya ufyatuaji na kugundulika kuwa wanatumia maji isivyo halali kwa kujiunganishia kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar  ws Salaam (DAWASA).  Makalla ambaye alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Matambo wa Maji wa Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani , pia alifanya msako wa kushitukiza kwa kampuni hizo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Ujenzi ya VA Tech Wabag Ltd, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Mitambo ya Maji ya Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani .Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Pintu Dutta.
Askari wa FFU wakilinda doria katika kiwanda cha ufatuaji tofali cha Ujenzi Solutions, Kimara Dar es Salaam
Moja ya mabomba linalodaiwa kuunganishwa kiholela kwenye bomba kuu la Ruvu Juu linaloleta maji  mjini na kampuni ya Ujenzi Solutions eneo la Kimara
Makalla akizungumza mbele ya Lori la Maji lililokamatwa likijazwa maji yanayodaiwa kuwa ya Dawass, katika kiwanda cha matofali cha Ujenzi Solutions
Pumpu iliyonaswa na Dawasa ikinyonyonya maji kutoka bomba kuu la Ruvu Juu eneo la Ubungo, Dar es Salaam
Makalla akiondoka katika kiwanda cha matofali cha Moto ambacho alisitisha shguli zake baada ya kubainika wakiiba maji ya Dawasa eneo la Ubungo.
Ramani ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, eneo la Mlandizi, Pwanik.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Wagani ambayo imepewa tenda ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu.
Makalla (wa pili kushoto) Mbunge wa Kihaha Vijijini, Hamoud Jumaa ( wa pili kulia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Halima Kihemba kulia, wakikagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo huo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top