|
Picha
zote za juu zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje
wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha cha Mikutano cha
Julius Nyerere ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya hafla ya kumuaga
Mhe. Rais. |
|
Rais
Kikwete akifunua kitambaa ambapo nyuma yake kuna picha ya Jengo la
Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje linalokusudiwa kuanza kujengwa hivi
karibuni. Rais Kikwete alifunua kitambaa hicho kuashiria kuanza ujenzi
wa jengo hilo. |
|
Rais Kikwete akipiga makofi kuonesha furaha yake kuwa Wizara ya Mambo ya Nje itapata ofisi za kisasa hivi karibuni |
|
Rais
Kikwete akiongozwa kuelekea ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya kufanya
hafla ya kumuaga. Wanaomuongoza ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa kulia kwa Rais Kikwete na Katibu
Mkuu, Balozi Liberata Mulamula. |
|
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akitoa neno la
kuwakaribisha wageni waalikwa akiwemo Rais Kikwete katika hafla ya
kumuaga. |
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akitoa
utambulisho wa wageni waalikwa wakiwemoWaheshimiwa Mabalozi waliostaafu. |
|
Balozi Mstaafu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa |
|
Watumishi
wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara/Vitengo, Waheshimiwa Mabalozi
wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa wameketi kwa ajili ya
kushuhudia matukio ya hafla ya kumuaga Rais Kikwete. |
|
Sehemu ya watumishi wa Wizara waliohudhuria hafla ya kumuaga Rais Kikwete |
|
Watumishi wa Wizara katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete |
|
Mtumishi
wa Wizara akisoma utenzi wa kumsifu na kumpongeza Rais Kikwete namna
alivyoongoza Taifa la Tanzania kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake
cha miaka 10 ambacho kinakamilika Oktoba 2015. |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K.Membe akisoma hotuba yake katika hafla
hiyo. Hotuba ya Waziri Membe iligusia mafaniki ambayo Serikali ya awamu
ya nne imeyapata katika kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na kuvutia
wawekezaji wakubwa, kuongeza uwakilishi nje ya nchi,kujenga ofisi za
kibalozi na utatuzi wa migogoro. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Membe wakionesha Tuzo aliyotunukiwa Rais Kikwte na Wizara ya Mambo ya Nje. |
|
Picha za juu zinaonesha zawadi mbalimbali ambazo Rais Kikwete amekabidhiwa wakati wa hafla hiyo |
|
Rais
Kikwete akiongea na watumishi wa Wizara na wageni waalikwa. Katika
mazungumzo yake Rais Kikwete alisisitiza umuhimu wa watumishi wa Wizara
kudumuisha na kuimarisha mahusiano mazuri na nchi zote duniani. Alisema
katika kipindi cha uongozi wake mafanikio makubwa ya kidiplomasia
yamepatikana hivyo ni vyema watumishi wa Wizara wakayaendeleza kwa
kiwango cha juu zaidi. |
|
Picha
ya pamoja kati ya Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Waziri Membe, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje,Wakuu wa Idara/Vitengo na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania
nje ya nchi |
|
Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment