Dkt. Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.
Mbunge
mteule jimbo la Nzega vijijini Dkt Hamisi Kigwangalla (CCM) ametoa
ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa
serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.
Kupitia
ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #SasaKaziTuChangamoto ya
Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka
ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John
Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri
kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii…kuna ‘expectation gap’
ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia
#MabadilikoYaKweli.
Nimesikia
kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za
serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika
kabisa kuwa kuna suluhisho bora zaidi ya hilo.
Inawashangaza
watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya hospitali
kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali
ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni
kuzuia uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali. Ninafahamu kwa
mfano, kuna tafiti zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya dawa
zilizopo ukilinganisha na pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya
utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa tofauti tofauti 850 (lines),
wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti tofauti takriban 3200!
Unaweza
kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa kwenye
hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu
kwa wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo.
Unaweza kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa
kutoka Muhimbili, na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa.
Na
nitakuuliza, zimepitia wapi pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi
kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka pharmacy, kwani pharmacy hiyo
ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu gani wa ‘wezi’ hao wa
madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
Nadhani njia hii ni too ‘mechanical’ na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha tatizo lingine ‘la usumbufu kwa wagonjwa’.
Nini kifanyike kudhibiti dawa zisikosekane kwenye mfumo wa afya?
1.Tuhakikishe
tuna dawa za kutosha kwenye Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuongeza
‘capacity’ yake kununua ‘lines’ nyingi zaidi za dawa kuliko ilivyo sasa,
ambapo MSD inaweza ku-supply only 65% ya mahitaji.
2.Bohari ijiendeshe kibiashara.
3.Tuweke
‘color code’ kwenye dawa zote za serikali kwenye bohari; mfano labda
dawa za serikali ziwe na rangi ya ‘pink’ pekee, na rangi hii iambatane
na ‘bar code’, na kuwe na ‘task force’ maalum ya ukaguzi wa pharmacy za
binafsi na ikitokea dawa ya serikali ikakutwa kwenye pharmacy yoyote ile
kuwe na adhabu kali.
4.Bohari
ya Dawa (MSD), kwa makubaliano maalum na hospitali husika, iruhusiwe
kufungua pharmacy zake kwenye hospitali zote nchini ili iuze moja kwa
moja kwa wateja. Tunaweza kuanza na hospitali chache za mfano – kama
Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Sekou Toure, Za Rufaa za Mikoa
na baadhi ya Wilaya, Vituo Vya Afya na Zahanati; Ili kuliko wateja wa
hospitali za serikali kwenda kununua dawa kwa bei ya kurusha kwenye
pharmacy za watu binafsi kule nje wanunue kwa bei nafuu ya serikali
ndani ya hospitali zetu.
SOURCE:MOBLOG
Post a Comment