Pichani
ni Mohammed Dewji alipokuwa mgeni rasmi wa tamasha la Simba Day,
akisalimiana na mmoja wa wadau kwenye jukwaa kuuna kulia ni Nyange
Kaburu. (Pichana Maktaba yetu).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Lile dili la
mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohamed Dewji kununua hisa katika klabu ya
Simba SC linaonekana kuiva baada ya makamu wa rais wa Simba kuzungumzia
dili hilo kuwa ni jambo nzuri la linafaida katika soka la sasa.
Akizungumza katika
kipindi cha E Sport kinachorushwa na E Fm, Makamu wa Rais wa Simba,
Geofrey Nyange Kaburu alisema jambo hilo wanalizungumzia kuangalia
uwezekano kama wanaweza kumruhusu bilionea Dewji kununua hisa katika
klabu hiyo.
Kaburu alisema katika
soka la sasa ni jambo nzuri kuruhusu wanachama wa klabu kununua hisa
ili timu iweze kupata mapato mengi zaidi na kuwa na uwezo zaidi wa
kujiendesha jambo linaloweza saidia timu kuwa imara kwa kuwa na uwezo wa
kufanya jambo lolote ambalo wanaona lina faida na timu.
“Kisoka la sasa
inakuwa ni vizuri kuuza hisa kwa mashabiki wetu ili timu iingize mapato
mengi na tuwe tunafanya biashara wakati tunazidi imarisha timu yetu na
swala la Dewji tunalo muda mrefu sana amekuwa akitaka tumuuzie hisa
tunalizungumzia,” alisema Kaburu.
Aliongeza kuwa baada
ya uongozi na washauri wao wa jinsi ya kuingiza fedha (EAG)
watawashirikisha na wanachama wa klabu na baada ya hapo watatoa tamko
juu ya kuanza kuuza hisa.
Taarifa za Bilionea,
Mohamed Dewji kutaka kuinunua klabu ya Simba zilianza kusambaa zaidi
baada ya kuzungumzia azma yake ya kuinunua Simba katika kipindi cha
Mkasi kinachorushwa na EATV na tangu hapo mashabiki mbalimbali wa klabu
hiyo kuanza kutoa maoni huku mashabiki wengi wakionekana kuridhia Dewji
kuinunua klabu yao wakiamini anaweza leta mabadiliko kwa kutangaza yupo
tayari kutoa Bilioni 20 kuiboresha Simba.
Post a Comment