Makonda akionesha kipeperushi kilichoelekeza namna ya kujiunga na huduma hiyo ya utoaji taarifa kwa njia ya simu za mkononi.…
Makonda akionesha kipeperushi kilichoelekeza namna ya kujiunga na huduma hiyo ya utoaji taarifa kwa njia ya simu za mkononi.
Makonda akijaribu kuandika ujumbe wa maeneno kutumia simu zake za mkononi kwa kuonesha wanahabari waliohudhuria mkutano huo.
Kipeperushi chenye maelezo kuhusu kampeni ya Sukuma Twende.
IKIWA sasa ni takribani wiki moja tangua
rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe
Magufuli aingie madarakani rasmi akiwa na kauli ya “Hapa Kazi Tu“ huku
akitembelea baadhi ya sekta za utumishi wa umma kwa kushtukiza, naye
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amekuja na kampeni aliyoipa
jina la “Sukuma Twende”.
Akizungumza na wanahabari leo ofisini
kwake jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Makonda
amesema lengo ni kuwasaidia wakazi wa Kinondoni kuondokana na matatizo
wanayokumbana nayo wanapokuwa wakihitaji huduma kwenye sekta za utumishi
wa umma.
Makonda amesema ujumbe huo utawawezesha
kufikisha malalamiko yao kwa kutoa taarifa na ushauri kupitia simu zao
za mkononi kwa kuandika ujumbe wa maneno kwenye simu ya mkononi moja kwa
moja pindi wanapoona watumishi wa sekta za utumishi wa umma wanazembea
au hawajali wananchi katika utoaji huduma.
“Kwa kupokea taarifa za wananchi
mbalimbali nitatumia dhamana niliyopewa na kuwafikishia wakuu wa idara
au sekta husika, lakini pia nina mamlaka ya kuwaonya kwa barua na hata
kuwasimamisha kazi, lengo langu ni kuongeza uwajibikaji katika sekta
mbalimbali serikalini,’’ alisema Makonda.
Aidha Makonda amesema kampeni hiyo ya
imeandaliwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Mobile,
hivyo wananchi watatuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno
Kinondoni au ‘KN’ wakiacha nafasi ukifuatiwa na ujumbe mfupi wa maneno
iwe ushauri au maoni na baada ya hapo utatuma kwenda namba 15404.
Uongozi huo umepanga kufikisha ujumbe
watakaoupokea kutoka kwa wananchi ndani ya wiki moja kwa atakaye kuwa
amelalmikiwa sana kutokana utendaje wake.
Aidha Makonda ametaja baadhi ya sekta
atakazoanza nazo ni Wizara ya Afya kwa maana ya hospitali zote zilizopo
Kinondoni, sekta ya ardhi, biashara, mahakama, Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na sehemu nyingine.
NA DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment