Diamond Platnumz amefanya collabo na kila msanii mkubwa wa Nigeria.
Ameshafanya
ngoma au kushiriki kwenye ngoma na P-Square, Davido, D’Banj, Tiwa
Savage, Iyanya, Waje, Kcee, Bracket, Flavour na wengine lakini ni msanii
mmoja tu mkubwa hajakutana naye kwenye wimbo wowote – Wizkid.
Wawili hao
walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye show ya Leaders Club
jijini Dar es Salaam, na picha zinaonesha kuwa tayari zimeiva, licha ya
ukweli kuwa huenda wamewahi kuwasiliana kabla ya hapo.
Baada tu ya
show yao ya Leaders wawili hao hawakuwa wachoyo kwa mashabiki wao
kuwaonesha kuwa mazungumzo ya kazi za baadaye yameanza.
Wikzid
alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Nana na kuandika, “Big up to
@diamondplatnumz for the love!! We link up soon!! #OneAfrica.”
Naye
Diamond alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Ojuelegba na kuandika,
“When they ask you, what was the name of the food you ate in Tanzania…
tell them “Ubwabwa na Kuku” @wizkidayo.”
Wizkid
atarejea tena December kwenye Fiesta na huenda kile mashabiki
wamekililia kwa muda mrefu kati ya mastaa hawa kitakamilika.
Post a Comment