Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Diamond Platnumz Kwa Hili la Baba yake Mzazi Hana Washauri?

Katika hili la mzazi wake wa kiume mimi binafsi limenigusa hasa kwa imani yangu ya dini. Siwezi kuhukumu moja kwa moja kwa maana sijui chanzo cha ugomvi wao wala status yao kwa sasa na pia MIMI SI HAKIMU, lakini nina haki ya kutoa maoni yangu hasa kumsaidia pia diamond ajitambue.

Katika hali ya kawaidia inatakiwa ingekuwa rahisi kama mzazi wako anapata msaada wako by then kila siku awe analalamika au tunamuona kwenye mitandao huo tayar ni udhaifu wako wewe mtoto kwa kuruhusu mzazi wako awe anakutia aibu wewe au familia yenu kwa ujumla. Kwa namna yoyote ni lazima suala la wazazi wako ukalipa umuhimu mkubwa sana katika maisha yako.

Katika mafundisho ya dini yanatufunza nini kuhusu wazazi?

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.

Akaamrisha ALLAH tabaaraka wata’la ihsani kwa wazazi wawili katika namna zote za wema, nao ni katika kauli [unapozungumza nao] pale aliposema [basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima]. Vivyo hivyo kuwafanyia wema katika matendo; kimwili na kimali kwa kauli yake aliposema: (Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma).
Na akanyanyua ubora wanapofika katika hali ya uzee, kisha akakataza kuwavunjia adabu na kuwatusi, achilia mbali kuwaacha wakiteseka.

UWAJIBU WA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAWILI:

Hakika ameamrisha Allah tabaaraka wata’la, na akawajibisha kwa njia ya wasia kuwafanyia wema wazazi wawili katika aya nyingi za qur’an. Pale ilipokuja amri ya wazi juu ya kuwatii, aliposema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili[1]

Ikaonesha wazi kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni wasia wa Allah kwetu. Bali akaliambatanisha jambo hilo la kuwafanyia wema wazazi wawili na twaa’ yake Allah tabaaraka wata’la pale aliposema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudie yeyote isipokuwa yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.[2]

Na kauli yake aliposema:
وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mwabudieni Allah wala msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili.[3]

Zikakusanya aya mbili hizi kuwa kufanyiwa wema wazazi wawili ni haqqi yao, bali akaifafanya haki hiyo kuwa ni ya pili baada ya tawheed yake Allah tabaaraka wata’la akionesha ukubwa wa jambo hilo [la kuwafanyia wema].

Amesema Al qurtwubiy [Allah amrehemu], kauli ya Allah “Na wazazi wawili kuwafanyia wema [ihsani]” maana yake ni:
برهما وحفظهما وصيانتهما وامتثال أوامرهما

Kuwafanyia wema na kuwahifadhi, kuwatunza na kutekeleza amri zao.

Katika kulisisitiza hilo, mpaka ikawa [wema kwa wazazi wawili] ni wenye kutangulizwa mbele hata kabla ya Sunnah za kujitolea kama vile Sunnah za kabla ya swala nk. Na kwa hili akaweka imamu muslim [Allah amrehemu] mlango katika swahih yake akiuita:
باب تقديم بر الوالدين على التطوع بالصلاة وغيرها

By the way mimi nimekubusha tu. Kama ni kweli mzazi hapati msaada basi ajitahidi kumsamehe, kama anapata msaada ila ndio umaarufu basi Diamond anisemehe maana binadamu tumeumbwa kukOsea. Na huu ni mwezi wa toba hakika atakuwa amenisamehe.

Asante.

Maskini Baba Diamond Platnumz, Azidiwa Ghafla

Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA
Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.

CHANZO CHAVUJISHA
Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI
“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe  hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA
Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.


ASAIDIWA NA WAHUDUMU
Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU
Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.

VIPIMO VINGINE
Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.
“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”

NGOZI IMEATHIRIKA
“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.


AMWAGA SHUKRANI
Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.


“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.
“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.


DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.

TUMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI
Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”

HARMONISE AACHIA NGOMA YAITWA ''BADO'' AKIMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ

Mwimbaji anaekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) kutoka Tanzania anayewakilisha kundi la Wasafi Classic Baby(Wcb),Harmonize ameachia wimbo wake wimbo mpya unaoitwa ‘BADO’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
 
 
SABABU YA KUREKODI WIMBO HUU.
Kwa singo mbili alizosikika Harmonize(Aiyola,Kidonda Changu) kwenye vyombo vya habari,jamii imekua ikimfananisha sana na Diamond kwenye uimbaji,ndipo siku moja Harmonize wakati akiimba Diamond alivutiwa na Melody ya wimbo huu na kusema hii itakua nafasi ya Watanzania kuwatofautisha kwenye uimbaji.
 
 
KUHUSU WIMBO WA BADO.
Harmonize alikaa na Diamond akamuuliza ni msichana gani alishamuumiza kiasi kwamba hawezi kumsahau,ingawa Diamond hakumwambia ni msichana gani,lakini akamwambia hiyo ni idea(Mwanga) mzuri wa kutunga wimbo ‘mkali’ Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Mtayarishaji(Producer) anaitwa Fraga na kabla ya kurekodi kwenye studio ya Wasafi,producer Fraga alimtumia midundo (Beat) 3 Harmonize  achague,ndipo akachagua beat ya wimbo huu na kurudi Wasafi Records kwa ajili ya kurekebishwa na kuanza kurekodiwa.
 
 
VIDEO YA WIMBO WA BADO.
Video ya wimbo huu imefanyika Afrika Kusini na Muongozaji(Director) anaitwa Nick ambaye ametengeneza video kadhaa ikiwemo Aiyola ya Harmonize mwenyewe,Make Me Sing ya Aka na Diamond,Love Boat Kcee na.Diamond,Walk it off ya Fid Q na nyingine nyingi

DIAMOND PLATNUMZ AMJIBU WEMA SEPETU BAADA YA WEMA KUCHONGA KUWA ANAJIKWEZA NA GARI YA BEI CHEE

Musa mateja
BAADA ya muigizaji nyota Wema Sepetu ‘kumtusi’ mpenziwe wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa kudhihaki zawadi ya bei chee ya gari aliyowahi kumnunulia, rais huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati aliibuka na kumjibu kuwa amefanya mambo ya ‘Kiswahili’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka mafanikio zaidi ya maisha yake.
“Kiukweli kabisa nampongeza Wema kwa kununua gari maana hiyo ndiyo ilikuwa mipango ya maisha yake, maneno anayosema kwamba mimi nilimnunulia gari la elfu thelathini ndipo nilipomuona wa ajabu. Sikuona umuhimu wa kunizungumzia pale.
“Hayo ndiyo mambo ya Kiswahili. Mimi siyo mtu wa kushindana kununua gari tena, maana hatua hiyo tayari nimeshapita, zaidi nawaza kupiga kazi na kujitengenezea maisha yangu mapya yatakayoweza kuifanya familia yangu iishi kwa raha na amani kipindi chote cha uhai wangu, najua kuna watu bado wanafikiria mimi ni limbukeni wa vitu kama zamani, kwa sasa sifikirii mashindano, ninaangalia kazi zinazoweza kuniingizia kipato tu,” alisema Diamond.
 Muigizaji nyota Wema Sepetu.
Katika pati aliyoiandaa hivi karibuni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Wema pamoja na mambo mengine, aliwaonyesha waalikwa zawadi ya gari aina ya Range Rover aliyojinunulia, akitoa maneno yaliyoonyesha kumponda Diamond, kwamba ameinunua kwa kiasi cha dola za Marekani 90,000 (karibu shilingi milioni 200 za Kitanzania), tofauti na watu wanaojikweza kwa ‘vigari vyao vya elfu thelathini’.
Source:GPL

LULU NA DIAMOND WAJA NA LAO JIPYA ,,,,JE WAJUA NI NINI ?


Hot gossip is that, Lulu Elizabeth Michael and Diamond Platnumz are in love secretly and Diamond's family has no problem about it. This comes after reports broke Diamond and his baby mama Zari The Boss Lady are in bad terms. Reports further say that Zari frequently saw Lulu's messages to Diamond ones of them being so romantic, and when Zari questioned Diamonds sisters kept telling Lulu and Diamond's are close friends for a long time.

Recently gossip and entertainment newspapers and blogs have been reporting Lulu and Diamond's so sudden closeness, even during Romy Jonesi birhday(Diamond's cousin) Lulu spent most of her time with Diamond and weeks later which was Diamond's birthday the two were together most of the time too.

When Diamond's sister Esma Platnumz approached by GPL paparazzi to give a comment on Lulu and Diamond's friendship she had this to say "yeah, you guys we have told you our brother(Diamond) has no problem with anyone, to Lulu he has no problem their relationship is open, first of all Lulu is beautiful, she is cool and she has what it takes to be someone's wife, we have no problem with her, if she and Diamond agree to one another we will welcome her warmly" said Esma

When Diamond asked he replied "please these are family issues, sometimes it is better to let somethings pass as they are, I have been close to Lulu for a long time, let it be that and end there"

After Diamond, paparazzi started looking for Lulu and finally the talented actress was spotted at Wema Sepetu's birthday over the weekend. When Lulu asked about being in love with Diamond she denied it claiming she can't do it because Diamond used to date Wema Sepetu "to date Diamond ! where can I start ?, and how could I have come here at Wema's birthday while Diamond is Wema's ex ?, nothing like that, he is my close friend"

 Leave that alone, Recently it was reported Lulu and Wema were in cold war because Wema was unhappy the way Lulu supports Diamond in every move let alone their closeness which frightened Wema who used to date Diamond and rumors suggest Wema still loves Diamond despite their separation. However Lulu attended Wema's Royal birthday over the weekend and they were snapped together.

Do you believe Lulu and Diamond are new couple in town ?

ZARI 'AMMAIND' ALIYEJICHORA TATUU YA DIAMOND

Hamida Hassan
Mahaba kweli hayazuiliki! Mrembo mmoja wa mjini ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alijikuta akikejeliwa na mpenzi wa Nasibu Abdul “Diamond’, Zarinah Hassan ‘Mama Tiffah’ baada ya mdada huyo kutupia picha mtandaoni akiwa amejichora tatuu yenye jina la Diamond kwenye matiti.

 Zarinah Hassan ‘Mama Tiffah’.
Baada ya mrembo huyo kuitupia picha hiyo na kujinasibu kuwa anampenda sana msanii huyo, Zari akaiona na kuonesha kuwa ana wivu kwa laazizi wake ‘alimtag’ Diamond kwa kuandika ‘Seen this?’ kisha kumkejeli demu huyo kwa kumwambia akae mbali ‘asilete shobo’.

Baada ya Zari kuandika hivyo, mrembo huyo alijikuta akipewa za chembe na wafuasi wa Diamond kwa kujipendekeza kwa mpenzi wa mtu.

MAMBO YAZIDI KUKUCHA COLLABO YA DIAMOND, ALLI KIBA NA WIZKID SASA INAKUJA KWA KASI.

Diamond Platnumz amefanya collabo na kila msanii mkubwa wa Nigeria.
Ameshafanya ngoma au kushiriki kwenye ngoma na P-Square, Davido, D’Banj, Tiwa Savage, Iyanya, Waje, Kcee, Bracket, Flavour na wengine lakini ni msanii mmoja tu mkubwa hajakutana naye kwenye wimbo wowote – Wizkid.
 
 
Wawili hao walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye show ya Leaders Club jijini Dar es Salaam, na picha zinaonesha kuwa tayari zimeiva, licha ya ukweli kuwa huenda wamewahi kuwasiliana kabla ya hapo.
 
Baada tu ya show yao ya Leaders wawili hao hawakuwa wachoyo kwa mashabiki wao kuwaonesha kuwa mazungumzo ya kazi za baadaye yameanza.
Wikzid alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Nana na kuandika, “Big up to @diamondplatnumz for the love!! We link up soon!! #OneAfrica.”

Naye Diamond alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Ojuelegba na kuandika, “When they ask you, what was the name of the food you ate in Tanzania… tell them “Ubwabwa na Kuku” @wizkidayo.”

Wizkid atarejea tena December kwenye Fiesta na huenda kile mashabiki wamekililia kwa muda mrefu kati ya mastaa hawa kitakamilika.

ANGALIA PICHA SITA KALI ZA SUPER STAR DIAMOND PLATINUMS AKIFANYA MAMBO YA AJABU KWENYE SHOW LEADERS








TASWIRA:WIZKID NA DIAMOND PLATNUMZ WAPATA LUNCH PAMOJA

Two African biggest music stars Nigerian Wizkid and Tanzanian Diamond Platnumz was snapped together having lunch as Wizkid had a music performance in Dar es salaam yesterday

Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top