Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa
katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
hospitalini hap oleo na kuwafariji wagonjwa.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya
ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali
ya kumsikitisha.
“ Rais amesikitishwa na
kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia
amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi
ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN
zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo
katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda
kutafuta huduma huko”. Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof.
Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia
kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye
anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako
atapangiwa kazi nyingine.
Balozi Sefue pia
amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya
wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za
uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia
wananchi kama ipasavyo.
Tayari Wizara ya
Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya
ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.
Hata hivyo Katibu
Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga
fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote
vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular
Maintenance).
Balozi Sefue pia
metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi
kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa
ipasavyo.
“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi
wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza
Balozi Sefue.
Rais Dkt.john Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa moyo
wauguzi katika hospitali ya taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya
ghafa kujionea hali halisi.
|
………Mwisho………
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
Post a Comment