Rais John Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha
BAADHI ya viongozi wa dini na jamii kwa ujumla wamemtaka Rais
wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli kuhakikisha anampata Waziri Mkuu
mchapa kazi na si vinginevyo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
Waliyasema hayo kwa vile wanaamini Waziri Mkuu ndiyo msimamizi mkuu wa mambo yote ya serikali, hivyo kukosea kwake kunaweza kukamfanya akashindwa kutekeleza ahadi zake.
Askofu wa Kanisa la Methodist jimbo la Dodoma, Joseph Bundara,
amesema ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima apatikane waziri mkuu
mwenye kusimamia maamuzi yasiyotetereka.
“Kwa sasa taifa letu wananchi wake wana hali mbaya kiuchumi hivyo
wanakabiliwa na umasikini wa kutupwa huku kundi la watu wadchache
wakijineemesha.
“Ili kuondoa hilo waziri mkuu ambaye ni msimamizi mkuu wa serikali
anatakiwa kuhakikisha anasimamia misingi ya utawara bora ikiwa ni
kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumiwa vizuri na kuwanufaisha
wananchi wote,” amesema Askofu Bundara.
Mbali na hilo alimtaka Rais Dk. Magufuli kuhakikisha anasitisha
matumizi mabaya ya rasilimali za serikali ambayo kwa hatua kubwa
yamesababisha nchi kuyumba na kuwafanya watanzania kuwa masikini.
Naye Hawa Makau, ambaye ni mkazi wilayani Mpwapwa, amesema ili taifa
liweze kusonga mbele ni lazima baraza la mawaziri liwe dogo na lenye
tija.
Aidha amesema rais huyo wa awamu ya tano anatakiwa kuwachagua
mawaziri na manaibu ambao ni wachapa kazi na asiangalie ukanda wala
kutoa nafasi hizo kwa upendeleo.
“Taifa hili lina watu wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa wa kufanya
kazi lakini mara nyingi hawapewi nafasi hizo kwa sababu ya viongozi wa
juu kulindana na kubebabana na wakati nafasi hizo upeana watoto wa
wakubwa.
“Nafasi za uongozi zitolewe kwa kuzingia ujuzi na uelewa wa mtu na
isiwe fadhila au kutomteua mtu mwenye uwezo kwa sasabu binafsi za
chuki,” alieleza Makua.
Licha ya uteuzi wa Mawaziri na Manaibu wake pia Makau alizungumzia
kuhusu suala la uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa kuwa nao ulenge kwa
vijana ambao wametoka vyuoni wenye taaluma badala ya kuendelea na
waliopo kwa sasa ambao hata wao wanaonekana kushindwa kazi.
“Mimi najiuliza maswali mengi ni kwanini wakuu wa wilaya na wakuu wa
mikoa wanachaguliwa hao hao tu wakati wapo vijana wengi wasomi na wenye
uwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo,” alieleza mwananchi huyo.
SOURCE:MwanaHalisi
Post a Comment