Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi ya
Serikali kuhusu upotoshaji wa baadhi ya vifungu vya sheria unaendelea
kufanywa na baadhi ya viongozi wa Kisiasa juu ya uhalali wa kuendelea
kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar.
Taarifa hiyo aliitoa katika kituo cha matangazo ya Shirika la Habari Zanzibar {ZBC-TV } Karume House Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania
kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika
madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka
pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.
Kauli hiyo
imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya
Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya
Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani
pamoja na Serikali yake.
Balozi Seif
aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashira
zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendelee kuwa watulivu na
kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema
Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika
kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi kwamba Rais aliyopo madarakani
atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula
kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi Seif
alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba
ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa
kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake
wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya
Kifungu hicho.
Alifafanua
kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya
Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo
masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za
Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya
Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana kwa
mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais
anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote
itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi Seif
alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na
sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa
nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa
ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema
Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa
kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata
ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza
kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na
kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi
ataendelea kuwepo madarakani mpaka pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika
madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha
Katiba.
Chanzo:Zanzinews
Picha na – OMPR – ZNZ.
Post a Comment