Uongozi
wa manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam umeanza kujipanga ili
kukabiliana na uwepo wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu ambapo
umeanza harakati za kutoa elimu ya usafi kwa wananchi.
Akizungumza na ITV baada ya kutia saini mkataba wa sh bilioni 1.3
kati ya manispaa hiyo na taasisi ya Water AID, mkuu wa wilaya hiyo Bi
Sophia Mjema amesema lengo ni hakuhakikisha manispaa hiyo inakuwa ya
mfano kwa Tanzania kwa usafi huku akitoa onyo kali kwa watu wanaofanya
uchafuzi wa mazingira.
Aidha mkurugenzi wa manispaa Temeke Bwana Fortdas amesema
atahakikisha fedha hizo zinatumika kwa lengo lililokusudiwa na si
vinginevyo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa shirika la Aater AIDS amesema lengo kuu
la msaada huyo ni kuhakiksha watu wanaishi kwenye mazingira safi na
salama pia kupata ajira kupitia mradi huo.
ITV
Post a Comment