Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka
watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam
kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia
watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa,
uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa
kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi
huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya
Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za
Ushuru na Bi. Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa
Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo
cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi
wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa
mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza
majukumu yake.
Loading...
Home
» JESHI LA POLISI
» Upotevu wa Makontena 349 Bandarini: Watu 12 Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment