Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


J1
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi  na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.
Picha na IKULU
J2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
J3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
J7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
J8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
J9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Arusha na Kilimanjaro waliofika Uwanja wa ndege wa KIA kumpokea.
J10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro (KIA). PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tarehe 03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili – Taveta – Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
02 Machi 2016
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top