Baada
ya waziri mkuu kutaja majina ya mawaziri wanne na naibu waziri mmoja
ambao hawajarudhisha fomu za Sekretariati ya maadili ya umma na kutakiwa
wawe wamerejesha fomu hizo mpaka saa kumi na mbili jioni ijumaa ya leo
mpaka sasa ni waziri mmoja aliyetii agizo hilo
Aliyerudisha fomu hizo ni waziri wa mambo ya nje,ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe.Balozi dkt.Augustine Mahiga
ambapo amekiri kuwa ni kweli alikuwa hajarudisha fomu hizo kutokana na
majukumu ya kazi yaliyokuwa yamembana
ITV pia imefanikiwa kuongea na waziri wa mambo ya ndani Charles
Kitwanga ambaye naye ametajwa kutorudisha fomu hizo ambapo ameshangaa
jina lake likitajwa wakati ameshazirudisha na kwa sasa ameelekea ofisi
za Sektretariati ya maadili kuwasilisha malalamiko yake
Pia ITV naibu waziri wa ofisi ya makamu wa rais,Muungano na
Mazingira Mhe.Luhaga Mpina ambapo amesema kuwa atawahisha kurudisha fomu
hizo kabla ya saa kumi na mbili jioni.
Post a Comment