Afisa
Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
(kulia) akimkabidhi msaada kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto Bi.
Jack Omary(kushoto) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha taifa cha
kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kurasini, hafla hii
imefanyika katika siku ya wapendanao. Misaada hyo imetolewa na vijana
wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam pamoja na
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
UN
Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha
Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa
watoto hao.
Vijana hao wa UN Club Tanzania Network
wanafanya kazi siku ya wapendanao nchi nzima za kusaidia jamii na vijana
wa jijini Dar es salaam wameungana na watoto wa kituo cha Kurasini kwa
kutoa msaada na wanafunzi hao wametoka katika shule za sekondari za
Zanaki, Azania, Benjamin na Jangwani.
Akizungumzia msaada huo, Afisa Ustawi wa
Jamii katika kituo hicho. Jack Omary aliwashukuru kwa kuwatembelea siku
ya wapendanao maana kuna watu wengine wanaitumia siku ya wapendanao
kwenye starehe na hata kutumia pesa bila kuangalia kuna watu wanahitaji
msaada.
Nae Stella kutoka UN Clubs Tanzania amesema
lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha Kurasini nikujumuika na
hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto wenye shida mbalimbali.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
(kushoto) akiwakabidhi misaada watoto wa Kituo cha Kurasini, katikati
ni mtoto Aboubakary Seif ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wenzake.
Alisema
inabidi kuwakumbuka hasa kwenye siku kama za wapendanao kwani kuna watu
wanatumia pesa nyingi kwenye starehe kuliko kutoa misaada kwa watoto
wenye mahitaji maalumu hasa wazee,walemavu na hata watoto yatima.
Mtoto Aboubakary Seif anayelelewa katika
kituo hicho cha Kurasini amewashukuru UN Clubs Tanzania Network Pamoja
na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Joyce Ndalichako kwa kuwaona kama watu katika jamii wanakubalika hasa
kwenye siku ya wapendanao.
Mwenyekiti
wa Jangwani Fema, Jeniffer Kayombo (kushoto) pamoja na Afisa habari wa
kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
wakiwakabidhi zawadi watoto wa kituo cha Kurasini jana ikiwa ni siku ya
wapendanao.
Amesema
wao wamesijsikia furaha kutembelewa na vijana wenzao na kuwapa moyo
hasa kwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Pia aliwaomba watu wengine wenye uwezo waje
kutoa msaada maana matatizo ni mengi na matatizo hayo yatatatuliwa kwa
misaada ya wadau mbalimbali.
Zuwena (kushoto) akimkabidhi mpira mtoto aliyewawakilisha wenzake kituoni hapo.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akizungumza jambo mbele ya watoto (hawapo pichani) walipowatembelea
watoto hao wenye mahitaji maalumu kwenye kituo cha Kurasini, jijini Dar
es Salaam katika siku ya wapendanao.
Mwenyekiti wa Jangwani Fema, Jeniffer Kayombo akiwaasa watoto kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akiwagawia watoto hao soda pamoja na biskuti ambapo Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
pamoja na vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es
salaam walitoa zawadi hizo.
Baadhi
ya vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam
kutoka katika shule za Sekondari za Jangwani, Zanaki, Benjamini na
Azania wakiwagawia zawadi watoto wenye mahitaji maalumu.
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Kurasini.
Hii ndio misaada iliyotolewa katika kituo cha kululea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akiwa kwenye picha ya pamoja na Umoja wa vijana wa youth advisory board
(FEMA YAB) walipotembelea watoto yatima katika kituo cha Kurasini
Jijini Dar es Salaam.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akiwa kweye picha ya pamoja na watoto wa kituoni hapo.
Picha ya pamoja.
Post a Comment