Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WANNE WAFARIKI AJALI YA TRENI UJERUMANI

Watu kadha wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya treni mbili za kubeba abiria kugongana katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani.


Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bad Aibling, takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.


Polisi wa Bavaria wameandika kwenye Twitter kwamba watu wanne wamefariki, 15 wameumia vibaya sana, 40 wakaumia vibaya na takriban watu 100 wana majeraha madogo.

Moja ya treni hizo ilitka kwenye reli baada ya ajali hiyo na mabehewa yake yakabingiria, vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema.


Inaaminika magarimoshi hayo yaligongana ana kwa ana.


Maafisa wa kutoa huduma za dharura wamefika eneo la ajalii na helikopta zinatumiwa katika uokoaji.


Barabara zilizo karibu na eneo hilo zimefungwa, sawa na njia ya reli kati ya miji ya Holzkirchen na Rosenheim.

CHANZO:BBC SWAHILI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top