Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MUENDELEZO WA HABARI:Ajali Mbaya Yatokea Asubuhi ya leo Dar es Salaam ..Daladala Lagongana na Lori la Kubebea Ng'ombe Eneo la Tabata MatumbiHabari za hivi punde.........

watu wanne wamefariki dunia na wengine 25 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi barabara ya Mandela eneo la Tabata Matumbi ,Jijini Dar es Salaam.

 Ng'ombe waliokuwa kwenye lori lililokuwa linaelekea Pugu Mnadani wakiwa chini baada ya ajali hiyo.
AJALI DAR: Daladala (DCM) lagongana na Lori la kubebea Ng'ombe eneo la Tabata Matumbi na kusababisha vifo na majeruhi (idadi bado). Barabara za kutoka na kwenda Buguruni zilifungwa kwa muda ili kupisha kazi ya uondoaji wa majeruhi  kutoka eneo la ajali.

Kutokana na ajali hiyo kutokea eneo la Tabata Matumbi kulisababisha foleni kubwa katika eneo zima la Tabata kuanzia maeneo ya Segerea kuelekea mjin na Ubongo kushindwa kupita kwa wakati na kufanya magari mengine kupitia Tabata Kimanga kuelekea  Ubungo.

HUko kote njiani kulikuwa na abiria wengi wakisubiria daladala ambazo zilikwama njiani kwenye foleni na abiria hao kutokujua kinachoendelea. Lakini hiyo ikawa neema kwa bodaboda wote ambao walionekana wakipishan kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kubeba abiria wenye kuwahi kazini. -----------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------------
MUENDELEZO WA HABARI: Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 16 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Amana,Ilala kwa matibabu zaidi.


Imeelezwa kwamba chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo saa 11.40 asubuhi  ni lori la mchanga lililokuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga daladala hilo kwa nyuma baada ya kukosa mwelekeo,hali hiyo ilifanya daladala hilo nalo kuligonga lori lililokuwa limepakia ng'ombe waliokuwa wanapelekwa pugu mnadani.


author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top