Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUBENEA:MAKONDA ALININYIMA KUZUNGUMZA AKISEMA RAIS WA KINONDONI AMEMALIZA


Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea.
............................
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea,  amepanda kizimbani na kukanusha kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 
Kubenea aliyasema hayo jana kwenye mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
Katika utetezi wake alioanza kuutoa jana, Kubenea alidai kuwa siku ya tukio, Makonda alimzuia kuzungumza na wananchi waliokuwa wamemwita, akidai kwamba yeye Rais wa Kinondoni na ameshazungumza, hivyo hakuna ruhusa ya mtu mwingine kusema. 
 
Akiongozwa na wakili wake, Peter Kibatala, Kubenea alidai: "Mheshimiwa hakimu, mimi sijatamka maneno hayo kwamba Makonda ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe cha kupewa bali nilimwambia wewe umeteuliwa na rais na mimi nimechaguliwa na wananchi… ndipo akaniambia yeye ni rais wa Kinondoni akishaongea hakuna ruhusa ya mtu mwingine kuongea."
 
Kubenea alidai kuwa Desemba 14, 2015 katika kiwanda cha TOOKU Garments Co. Ltd, kilichoko Mabibo External, Ubungo, wakati wa  mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda hicho alimwambia mkuu huyo wa wilaya kwamba hawezi kufunga mkutano bila  yeye mbunge kuzungumza kwa sababu ni mwakilishi wa wananchi.
 
“Makonda alinijibu kwamba kila anapozungumza yeye ndiye mtu wa mwisho kwa sababu ni rais wa Kinondoni anachokiamua hakuna kingine” alidai Kubenea.
 
Akifafanua zaidi, mshtakiwa alidai kuwa alimweleza Makonda  kwamba yeye ni mbunge na amechaguliwa na wananchi kwa zaidi ya kura 17,000 hivyo ni lazima aheshimu uwapo wake katika tukio hilo.
 
Alidai pamoja na kujieleza kwamba aliitwa na wananchi kwenye mkutano huo, DC Makonda hakumpa nafasi ya kuzungumza na badala yake alimwamuru Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi  Magomeni, Denis Mujumba, kumkamata apelekwe kupumzishwa.
 
“Kamanda Mujumba alinifuata na kunieleza kwamba niko chini ya ulinzi. Aliniamuru ninyooshe mikono, nilimhoji ananikamata kwa kosa gani au kwa kuagizwa na mkuu wa wilaya?” alidai Kubenea.
 
Pia DC (Mkuu wa Wilaya) Makonda aliamuru raia wa China anayedaiwa kunyanyasa  wafanyakazi hao akamatwe na achunguzwe.
 
Awali, Kubenea alidai mahakamani hapo kuwa siku ya tukio, majira ya saa tano asubuhi, alifika kwenye kiwanda hicho, baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mgomo na wakazungumza hadi saa 9.30 jioni.
 
Alidai akiwa kiwandani hapo alionana na uongozi wa kiwanda hicho,  uongozi wa chama cha wafanyakazi juu ya madai mbalimbali ikiwamo nyongeza ya mshahara na kwamba wakakubaliana kuongeza asilimia tano toka Sh 100,000.
 
Alibainisha kuwa wakiwa bado katika mkutano huo, walisikia ving'ora na wafanyakazi waliokuwapo nje wakiamini ni Rais Dk. John Magufuli amekwenda kimbe ni Makonda ameongozana na askari polisi ambao idadi yao hawezi kuikumbuka.
 
Kubenea alidai kuwa alitambia uwapo wake, akampa taarifa na mahali walipofikia na kwamba Mkonda alimweleza kuwa ''Mbunge hawa watu ni wahuni twende ndani ya kikao tukapambane.
 
''Tukiwa ndani kikao kilianza upya, muafaka haukupatikana na Makonda aliahidi kesho yake Desemba 15, 2015 kuwapeleka waziri wa viwanda na biashara na waziri wa kazi na ajira na akwapa nafasi watu wengine kuongea yeye akamnyima.
 
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mashahidi watatu wa upande wa mashtaka ambao ni  Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi,  ASP Denis Mujumba (39), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda pamoja na askari PC Gabriel kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi hiyo inayomkabili Kubenea na kuufunga.
 
Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kuwa Desemba 14, 2015 katika kiwanda cha Tooku Garments Co.Ltd kilichopo Mabibo External   alimtolea lugha ya matusi DC Makonda  kuwa wewe ni kibaka, mjinga, mpumbavu tena umeteuliwa kwa kupewa.
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top