|
Pichani
Balozi Muhammad Tayeb, Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya
Saudi Arabia akimkaribisha Bw. Suleiman Saleh, Konseli Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Jeddah, na kufanya nae mazungmzo kuhusu
mahusiano baina ya Saudi Arabia na Tanzania.
Kwa mujibu wa Balozi Tayeb, kusainiwa kwa
makubaliano hayo kumefungua ukurasa mpya wa mahusiano baina ya Saudi Arabia na
Tanzania na hakusita kuonyesha furaha yake kutokana nakuainishwa maeneo
mahususi ya mashirikiano katika sekta za uchumi, uwekezaji na
biashara. Kwa upande wake Bw. Saleh alimshukuru Balozi
Muhammad Tayeb kwa kumkaribisha Ofisini kwake na alifarijika na upendo
alionyesha Balozi huyo kwa Tanzania ambapo alichukwa fursa hiyo
kumualika kutembelea Tanzania kujionea vivutio vya utalii Tanzania Bara na
Visiwani ambapo aliukubali mwaliko huo na kuahidi kutembelea Tanzania yeye na
familia yake mwezi Julai, 2016. |
========================================
Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Bw. Suleiman Saleh, Jumanne
Machi 29, 2016, amekaribishwa rasmi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi
Arabia alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi Muhammad A. Tayeb,
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara hiyo.
Balozi Tayeb alimpokea Bw. Saleh Ofisini kwake
Jeddah na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuimarisha mahusiano
baina ya Saudi Arabia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kusainiwa
hivi karibuni Ikulu, Dar-es-Salaam, makubaliano ya mashirikiano baina ya nchi
hizo mbili. Makubaliano hayo ambayo yalisainiwa na Mhe. Adil Jubeir,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia na Mhe. Balozi Augustine Mahiga, Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, yalishuhudiwa pia na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment