Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA: MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA EACRais wa Zanzibar Mhe.Dkt.Ally Mohamed Shein akisalimiana na Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Katiba na Sheria mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwaajili ya kuhudhuria Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika Mashariki

Rais Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein akivipongeza vikundi vya wacheza ngoma vilivyokuja kumpokea uwanjani hapo.

Kikundi cha ngoma cha wanawake kikimpokea kwa shangwe Mhe. Rais wa Zanzibar.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwaajili ya kuhudhuria Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe  wa pili kulia aliongoza mapokezi ya kiongozi huyo.

Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akisalimiana na viongozi wa jeshi ambao walikuja kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Charles Kitwanga akiwa ameambatana naye mara baada ya kumpokea.


Kaimu Mkuu wa Itifaki Bw. James Bwana akitoa maelekezo kwa Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambaye alimpokea Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata ambaye aliwasili kwaajili ya kushiriki mkutano huo.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya  Mhe.John Haule mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.

Mhe, Rais Uhuru Kenyata akisalimia vikundi vya ngoma havipo pichani vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.

Wakuu wa Nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika Mkutano  wa 17 ambapo katika Mkutano huo Sudan ya kusini nayo imepata usajili wa uanachama katika umoja huo baada ya maombi yake kujadiliwa na kukubaliwa.


Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo akihutubia katika Mkutano, ambapo ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki Mkutano huo tangu ashinde uchaguzi na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu Mkuu mteule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw, Liberat Mphumukeko kutoka nchini Burundi akiapa katika mkutano huo wa wakuu wa nchi mara baada ya uteuzi wake.

Bw. Liberat Mphumukeko akipewa pongezi na Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa nchini Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga mara baada ya kukamilisha taratibu za kiapo.

Waheshimiwa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wameshika Hati ya kimataifa ya kusafiria ndani ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambapo uzinduzi wa hati hiyo ulifanyika katika mkutano huo.
Kijana Simon Moleli kutoka shule ya Sekondari ya Mzumbe ambaye alikuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya uandishi wa insha ya Afrika Mashariki mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi na fedha vikiwa ni tuzo kwa ushindi alioupata.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Innocent Shio wa pili kutoka kushoto akifatilia mkutano.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top