|
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia)
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO kwa upande wa Afrika,
Bw. Firmin Matoko walipokutana kwa ajili ya mazungumzo kwenye Ofisi za
Wizara ya Mambo ya Nje.
|
|
Balozi
Mushy akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO kwa
upande wa Afrika, Bw. Firmin Matoko. Mazungumzo hayo pamoja na Mambo
mengine yalijikita katika vipaumbele vya UNESCO ambavyo ni elimu na
jinisia. Kwa upande wa elimu, Balozi Mushy alieleza hatua ya Serikali ya
awamu ya tano kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari. Kuhusu
jinsia, alieleza hatua ya Serikali ya kujumuisha wanawake katika nafasi
za uongozi ikiwa ni pamoja na kuimchagua Makamu wa Rais Mwanamke wa
kwanza. Mwingine katika picha ni Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania,
Bi. Zulmira Rodrigues. |
|
Wajumbe wakiendelea na mazungumzo |
|
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Ngusekela Nyerere na Afisa wa UNESCO wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo. |
|
Balozi Mushy akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Matoko. |
|
Picha ya pamoja. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment