Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAKENYA WASABABISHA TTB KUTOA KAULI KUHUSU OLDUVAI GORGE


BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao kuhusu eneo la Olduvai Gorge kuwepo nchini Kenya, ikisisitiza kuwa eneo hilo lipo Tanzania.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TTB Dar es Salaam jana ilisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikifuatilia video iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya. 
 
 
Ilisema kimsingi eneo hilo la Olduvai Gorge liko katika Bonde la Ufa katikati ya Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.
 
 
Ilisema Video hiyo imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.
 
 
Taarifa ilibainisha kuwa TTB kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vya utalii imeshtushwa na video hiyo iliyojaa upotoshwaji ambao wanaamini mbali ya malengo mengine ililenga kuchafua kazi nzuri inayofanywa na TTB kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.


Iliongeza kuwa TTB inapinga vikali upotoshwaji huo uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana.

Ilifafanua kuwa TTB inapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar na nyinginezo, Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. 
 
TTB inatoa wito kwa watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi zao za kuvitangaza vivutio vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo upotoshaji kuhusu Tanzania unapotokea ndani ya nchi au nje.
Mwisho.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top